Skip to content

Mwanamke kapata ajali, na alikuwa mwanzoni mwa mimba yake, mimba ikatoka baada ya kutokwa na damu nyingi, je inajuzu kwake kufungua, au anaendelea kufunga? Akifungua je atapata dhambi?

السؤال

Swali la 1:

Mwanamke kapata ajali, na alikuwa mwanzoni mwa mimba yake, mimba ikatoka baada ya kutokwa na damu nyingi, je inajuzu kwake kufungua, au anaendelea kufunga? Akifungua je atapata dhambi?

س28: امرأةٌ أصيبت في حادثةٍ، وكانت في بداية الحمل، فأسقطت الجنين إثر نزيفٍ حادٍّ، فهل يجوز لها أن تفطر، أو تواصل الصّيام؟ وإذا أفطرت فهل عليها إثمٌ؟

الجواب

Jawabu la 1:

Tunasema: Hakika mjamzito hatokwi na damu ya hedhi, kama anavyosema Imam Ahmad: Wanawake wengi hujua ujauzito kwa kukatika hedhi, na hedhi kama walivyosema Wanachuoni, ameiumba Allah -Mtukufu- kwa hekima ya kuwa ni chakula cha mtoto aliye tumboni, mimba itakapoanza hedhi hukatika.

Lakini baadhi ya wanawake inaweza ikaendelea kwake damu ya hedhi kama kawaida kama ilivyokuwa kabla ya mimba, huyu atahukumiwa kuwa hedhi yake ni hedhi ya kawaida, kwa sababu hedhi kwake iliendelea na wala haikuathirika na mimba, hedhi hii itamzuia na yale yote ambayo yanayozuiwa na hedhi ya siku zote ya mwanamke asiyemjamzito, hivyo, itawajibisha yale ambayo yanawajibika kwa mwenye hedhi, na itadondosha yale yote ambayo yanadondoshwa na hedhi ya kawaida (ikiwemo swala n.k)

Na kwa ufupi ni kwamba: Damu inayomtoka mjamzito iko katika aina mbili:

Aina moja wapo inahukumiwa kuwa ni hedhi, nayo ni ile ambayo inaendelea kutoka kwake kama ilivyokuwa ikitoka kabla ya mimba, basi maana ya jambo hili ni; Mimba haijamuathiri, hii itakua ni hedhi ya kawaida.

Na aina ya pili, ni damu inayotoka wakati wa mimba, ima kwa sababu ya ajali, au alibeba kitu kizito, au kudondoka toka juu ya kitu fulani na mfano wake, damu hii si hedhi, bali ni damu ya ugonjwa.

kwa hiyo, haimzuii damu hii kuswali, wala kufunga, bali anakuwa katika hukumu ya wanawake waliotwaharika.

Lakini ajali ikisababisha mtoto kushuka au mimba ambayo iliyokuwa tumboni, atakuwa kama walivyosema wanachuoni: Mimba ikitoka na imebainika kwake umbile la mwanadamu, basi damu itakayotoka baada ya kutoka mtoto itahesabika kuwa ni damu ya uzazi, ataacha kuswali, na kufunga, na mumewe atajitenga naye mpaka atwaharike.

Na akitoka mtoto ambaye hajakamilika basi haizingatiwi kuwa ni damu ya uzazi, bali ni damu iliyoharibika, haimzuii mwanamke kuswali, wala kufunga, wala kingine chochote.

wamesema Wanachuoni: Muda mchache ambao kinabainika kiumbe: Ni siku themanini na moja; kwa sababu mtoto yupo tumboni kwa mama yake.

Kama alivyosema Abdullah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- Ametuhadithia mkweli mwenye kusadikishwa, akisema: "Hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake katika tumbo la mama yake siku arobaini, kisha linakuwa pande la damu mfano wa siku hizo, kisha linakuwa pande la nyama mfano wa siku hizo, kisha hutumwa Malaika na anaamrishwa kuandika mambo manne; kuandika riziki yake, kifo chake, muovu au mwema".

Na wala haiwezekani kuumbwa kabla ya siku hizo, mara nyingi kiumbe hakibainiki kabla ya siku tisini, kama walivyosema baadhi ya Wanachuoni.

ﺟ28: نقول: إن الحامل لا تحيض، كما قال الإمام أحمد:

"إنما تعرف النّساء الحمل بانقطاع الحيض".

والحيض -كما قال أهل العلم- خلقه الله تبارك وتعالى لحكمة غذاء الجنين في بطن أمّه، فإذا نشأ الحمل انقطع الحيض.

لكن بعض النّساء قد يستمرّ بها الحيض على عادته كما كان قبل الحمل، فهذه يحكم بأن حيضها حيضٌ صحيحٌ؛ لأنه استمر بها الحيض، ولم يتأثر بالحمل، فيكون هذا الحيض مانعًا لكلّ ما يمنعه حيض غير الحامل، وموجبًا لـما يوجبه، ومسقطًا لـما يسقطه.

والحاصل: أن الدم الّذي يخرج من الحامل على نوعين:

نوعٌ يحكم بأنه حيضٌ، وهو الّذي استمر بها كما كان قبل الحمل، فمعنى ذلك: أن الحمل لم يؤثّر عليه، فيكون حيضًا.

والنوع الثاني: دمٌ طرأ على الحمل طروءًا، إما بسببٍ حادثٍ، أو حمل شيءٍ، أو سقوطٍ من شيءٍ ونحوه، فهذه دمها ليس بحيضٍ، وإنما هو دم عرقٍ،

وعلى هذا فلا يمنعها من الصلاة، ولا من الصوم، بل هي في حكم الطاهرات.

ولكن إذا لزم من الحادث أن ينزل الولد أو الحمل الذي في بطنها فإنها على ما قال أهل العلم: إن خرج وقد تبين فيه خلق إنسانٍ فإن دمها بعد خروجه يعدّ نفاسًا، تترك فيه الصلاة والصوم، ويتجنبها زوجها حتى تطهر.

وإن خرج الجنين وهو غير مخلّقٍ فإنه لا يعتبر دم نفاسٍ، بل هو دم فسادٍ، لا يمنعها من الصلاة، ولا من الصّيام، ولا من غيرهما.

قال أهل العلم: وأقلّ زمنٍ يتبين فيه التخليق: واحدٌ وثمانون يومًا؛ لأن الجنين في بطن أمّه، كما قال عبد الله بن مسعودٍ رضي الله عنه: حدثنا رسول الله ﷺ وهو الصادق المصدوق، فقال:

«إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُبْعَثُ إِلَيْهِ الْمَلَكُ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ، فَيُكْتَبُ رِزْقُهُ، وَأَجَلُهُ، وَعَمَلُهُ، وَشَقِيٌّ أَوْ سَعِيدٌ» [1]،

ولا يمكن أن يخلق قبل ذلك، والغالب أن التخليق لا يتبين قبل تسعين يومًا، كما قال بعض أهل العلم.

[10] رواه البخاري، كتاب أحاديث الأنبياء، باب خلق آدم وذريته (3333)، ومسلم، كتاب القدر، باب كيفية خلق الآدمي في بطن أمه (1) (2643).