Skip to content
يُونس /

Aya 106

10 : 106
يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 106

وَلَا تَدۡعُ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَۖ فَإِن فَعَلۡتَ فَإِنَّكَ إِذٗا مِّنَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Na wala usiwaombe wasio kuwa Mwenyezi Mungu ambao hawakufai kitu wala hawakudhuru. Ukifanya hivyo basi utakuwa miongoni mwa walio dhulumu.

Explanation & meanings · 1
  1. Wala usimkimbilie kwa kumwomba na kumuabudu yeyote asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Hao hawakuletei manufaa wala madhara. Ukifanya hayo inakuwa umekwisha ingia miongoni mwa washirikina walio dhulumu. Na anayo katazwa Nabii, ndio wanakatazwa umma wake wote. Na hivyo ndio ukomo wa kukanya. Kwani kumkanya ambaye hayumkiniki kutenda anacho kanywa, ndio hadi ya kukanya.