Skip to content
التوبَة /

Aya 65

9 : 65

Aya 65 of التوبَة (9 : 65). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

التوبَة Aya 129
Sura · التوبَة
Kiswahili · Barawani
9 : 65

وَلَئِن سَأَلۡتَهُمۡ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلۡعَبُۚ قُلۡ أَبِٱللَّهِ وَءَايَٰتِهِۦ وَرَسُولِهِۦ كُنتُمۡ تَسۡتَهۡزِءُونَ

Na ukiwauliza, wanasema: Sisi tulikuwa tukipiga porojo na kucheza tu. Sema: Mlikuwa mkimfanyia maskhara Mwenyezi Mungu na Ishara zake na Mtume wake?

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Mtume! Kuwa na yakini kwamba, baada ya kwisha fedheheka mambo yao hawa wanaafiki, ukawauliza sababu ya kuitia ila Dini na kumfanyia kejeli Mwenyezi Mungu na Ishara zake, wao hutoa udhuru kwa kusema: Tulikuwa tunapiga porojo na tukicheza tu! Waambie: Vipi inakufalieni kupiga porojo na kucheza kwa kumfanyia maskhara Mwenyezi Mungu na Aya zake na Mtume wake?