6 : 82
ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَمۡ يَلۡبِسُوٓاْ إِيمَٰنَهُم بِظُلۡمٍ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلۡأَمۡنُ وَهُم مُّهۡتَدُونَ
Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka.
Explanation & meanings · 1
- Wanao muamini Allah, (Mwenyezi Mungu), na wasiichanganyishe imani yao hii na ibada ya yeyote asiye kuwa Yeye - hao tu ndio wenye haki ya kupata utulivu, na ni wao tu ndio walio ongoka kuishika Njia ya Haki na Kheri.