Skip to content
يُونس /

Aya 107

10 : 107
يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 107

وَإِن يَمۡسَسۡكَ ٱللَّهُ بِضُرّٖ فَلَا كَاشِفَ لَهُۥٓ إِلَّا هُوَۖ وَإِن يُرِدۡكَ بِخَيۡرٖ فَلَا رَآدَّ لِفَضۡلِهِۦۚ يُصِيبُ بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۚ وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Na Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapana wa kukuondolea ila Yeye. Na akikutakia kheri, basi hapana awezaye kurudisha fadhila yake.Huifikisha kwa amtakaye katika waja wake, na Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Yakikusibu madhara kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hapana wa kuyaondoa ila Yeye. Na akikujaalia kheri hapana anaye weza kukunyima yeyote. Kwani yeye anagawa kheri kuwapa waja wake kwa fadhila yake. Na Yeye Subhanahu ni Mkunjufu wa maghfira, Mkuu wa rehema.