Skip to content
المَائدة /

Aya 61

5 : 61
المَائدة Aya 120
Sura · المَائدة
Kiswahili · Barawani
5 : 61

وَإِذَا جَآءُوكُمۡ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا وَقَد دَّخَلُواْ بِٱلۡكُفۡرِ وَهُمۡ قَدۡ خَرَجُواْ بِهِۦۚ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا كَانُواْ يَكۡتُمُونَ

Na wanapo kujieni husema: Tumeamini. Lakini hakika wao wameingia na ukafiri wao, na wametoka nao pia. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi kabisa wa yote wanayo yaficha.

Explanation & meanings · 1
  1. Wanaafiki wakikujia husema uwongo, na hukwambia: Tumeamini. Nao wamekuingilia na hali ni makafiri, na wametoka kwenu nao ni makafiri vile vile! Na Mwenyezi Mungu anaujua vyema unaafiki wanao uficha. Na Yeye ndiye atakaye waadhibu.