Skip to content
الزُّمَر /

Aya 38

39 : 38

Aya 38 of الزُّمَر (39 : 38). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الزُّمَر Aya 75
Sura · الزُّمَر
Kiswahili · Barawani
39 : 38

وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّنۡ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُۚ قُلۡ أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ إِنۡ أَرَادَنِيَ ٱللَّهُ بِضُرٍّ هَلۡ هُنَّ كَٰشِفَٰتُ ضُرِّهِۦٓ أَوۡ أَرَادَنِي بِرَحۡمَةٍ هَلۡ هُنَّ مُمۡسِكَٰتُ رَحۡمَتِهِۦۚ قُلۡ حَسۡبِيَ ٱللَّهُۖ عَلَيۡهِ يَتَوَكَّلُ ٱلۡمُتَوَكِّلُونَ

Na ukiwauliza: Ni nani aliye ziumba mbingu na ardhi. Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu. Sema: Je! Mnawaonaje wale mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru, wao wanaweza kuniondolea dhara yake? Au akitaka kunirehemu, je, wao wanaweza kuzuia rehema yake? Sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Kwake Yeye wategemee wanao tegemea.

Explanation & meanings · 1
  1. Na ninaapa, lau ungeli wauliza, wewe Muhammad, hawa washirikina: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka wangeli sema: Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba. Ewe Muhammad, waambie: Mmezingatia mkawaona hao miungu mnao washirikisha na Mwenyezi Mungu, wanaweza kuniondolea madhara ikiwa Mwenyezi Mungu anataka kunidhuru? Au wanaweza kunizuilia rehema yake akitaka inifikie? Ewe Muhammad! Waambie: Anaye nitosheleza kwa kila kitu ni Yeyey peke yake, si mwenginewe, ndiye Yeye wanaye mtegemea wote wanao tegemea na kumwachilia kila kitu.