Basi tambua kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni wamuabudu yeye na wala wasimshirikishe na kitu chochote, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu asimwaadhibu yeyote ambaye hajamshirikisha yeye na chochote
Kutoka kwa Muadhi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema:
Nilikuwa nimepanda Punda nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Punda akiitwa Ufairu, akasema Mtume: "Ewe Muadhi hivi unazijua haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake na zipi haki za waja kwa Mwenyezi Mungu?" Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: " Basi tambua kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni wamuabudu yeye na wala wasimshirikishe na kitu chochote, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu asimwaadhibu yeyote ambaye hajamshirikisha yeye na chochote" Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwanini nisiwape watu habari hii? Akasema Mtume: "Usiwape habari hii kwani watabweteka".
كُنْتُ رِدْفَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى حِمَارٍ يُقَالُ لَهُ عُفَيْرٌ، فَقَالَ: «يَا مُعَاذُ، هَلْ تَدْرِي حَقَّ اللَّهِ عَلَى عِبَادِهِ، وَمَا حَقُّ العِبَادِ عَلَى اللَّهِ؟»، قُلْتُ: اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «فَإِنَّ حَقَّ اللَّهِ عَلَى العِبَادِ أَنْ يَعْبُدُوهُ وَلا يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَحَقَّ العِبَادِ عَلَى اللَّهِ أَنْ لا يُعَذِّبَ مَنْ لا يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا»، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ أَفَلاَ أُبَشِّرُ بِهِ النَّاسَ؟ قَالَ: «لا تُبَشِّرْهُمْ، فَيَتَّكِلُوا».
Anaziweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja ni kuwa wamuabudu yeye peke yake na wala wasimshirikishe yeye na kitu chochote. Na kuwa haki za waja kwa Mwenyezi Mungu ni kutowaadhibu wenye kumpwekesha ambao hawamshirikishi yeye na chochote. Kisha Muadhi akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwa nini nisiwape watu habari hii njema ili wafurahi kwa jambo hili bora? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamkataza kwa kuogopea kuwa watategemea habari hiyo.
...:
Kumewekwa wazi haki za Mwenyezi Mungu ambazo amewajibisha kwa waja wake, nazo ni kumuabudu yeye, na wasimshirikishe na kitu chochote.
Kumewekwa wazi haki ya waja kwa Mwenyezi Mungu ambayo ameiwajibisha yeye mwenyewe kwa fadhila zake na neema zake, na haki hiyo ni kuwaingiza peponi, na kutowaadhibu.
Katika hadithi hii kuna bishara njema na kubwa kwa wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, wale ambao hawamshirikishi Mwenyezi Mungu Mtukufu na kitu chochote, na kuwa mafikio yao ni kuingia peponi.
Alihadithia Muadhi hadithi hii kabla ya kufa kwake; kwa kuogopea kuingia kwenye madhambi ya kuficha elimu.
Kuna tahadhari ya kuacha kueneza baadhi ya hadithi kwa baadhi ya watu kwa kuogopea mtu kutofahamu maana yake; na hofu hiyo ni kwa yule ambaye hana matendo wala hayupo kwenye sheria miongoni mwa sheria.
Wafanyaji maasi wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu wapo chini ya utashi wa Mwenyezi Mungu, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe, kisha mafikio yao yatakuwa peponi.
Swahiih Al Bukhaariy (4/ 29) (2856).
Swahiih Muslim (1/ 58) (30).
(1/ 627).
Zaidi (5)
المحكم لابن سيده (10/26).
المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 203).
فتح الباري (11/340.
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (1/ 623).
عمدة القاري شرح صحيح البخاري (14/ 148).
Imenukuliwa katika vitabu
12 Vitabu- Itikadi sahihi na mambo yanayopingana nayo.((Haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, ni wamuabudu yeye na wala wasimshirikishe na kitu chochote)).
- Itikadi sahihi na mambo yanayopingana nayo."Hivi unajuwa ni ipi haki ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu?" Akasema Muadh: Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajuwa zaidi. Akasema Mtume - rehema na amani ziwe juu yake -: Haki za Mwenyezi Mungu kwa
- Kitabu cha Tauheed {upwekeshaji}كتاب التوحيد للشيخ محمد بن عبد الوهابHaki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja ni kumuabudu yeye na wala wasimshirikishe na chochote, na haki ya waja juu ya ALLAH ni kuto kumuadhibu yule asiyemshirikisha yeye na chochote.
Zaidi (9)
- العقيدة الصحيحةدروس العقيدة الصحيحة«فَإِنَّ حَقَّ اللَّهِ عَلَى العِبَادِ: أَنْ يَعْبُدُوهُ وَلَا يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَحَقَّ العِبَادِ عَلَى اللَّهِ: أَنْ لاَ يُعَذِّبَ مَنْ لَا يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا»
- حراسة التوحيدالعقيدة الصحيحة وما يضادها «حَقُّ اللهِ عَلَى العِبَادِ أَن يَعْبُدُوهُ وَلَا يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا» [2].
- حراسة التوحيدإقامة البراهين على حكم من استغاث بغير الله«حَقُّ اللهِ عَلَى العِبَادِ أَنْ يَعْبُدُوهُ وَلَا يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا».
- خذ عقيدتك من الكتاب والسنة الصحيحة«حق العباد على الله أن لا يُعذِّبَ مَن لَا يشركُ به شيئًا»
- مجموعة زاد التربية الإسلامية (1)، والسيرة النبوبة (1)، والعقيدة (1)، والفقه (1)التربية الأسلامية 1قال: «فإن حق الله على العباد أن يعبدوه ولا يشركوا به شيئًا، وحق العباد على الله ألا يعذب من لا يشرك به شيئًا»
- مجموعة زاد التربية الإسلامية (1)، والسيرة النبوبة (1)، والعقيدة (1)، والفقه (1)التربية الأسلامية 1«حقُّ اللهِ على العِبادِ أنْ يعْبُدُوهُ ولا يُشْرِكُوا بِهِ شيْئًا...»
- مشروع منهاج زادكزادك 2 طالب نهائي«يَا مُعَاذُ، هَلْ تَدْرِي حَقَّ اللهِ عَلَى عِبَادِهِ؟ وَمَا حَقُّ العِبَادِ عَلَى اللهِ؟». قُلْتُ: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. قَالَ: «فَإِنَّ حَقَّ اللهِ عَلَى العِبَادِ أَنْ يَعْبُدُوهُ وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَحَقَّ العِبَادِ ع
- نبراس طالب (3)نبراس طالب 3«يَا مُعَاذُ، هَلْ تَدْرِي حَقَّ اللهِ عَلَى عِبَادِهِ، وَمَا حَقُّ العِبَادِ عَلَى اللهِ؟»، قُلْتُ: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «فَإِنَّ حَقَّ اللهِ عَلَى العِبَادِ أَنْ يَعْبُدُوهُ وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَحَقَّ العِبَادِ ع
- نبراس طالب (3)نبراس طالب 3«فَإِنَّ حَقَّ اللهِ عَلَى العِبَادِ أَنْ يَعْبُدُوهُ وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا»