Skip to content
الإسرَاء /

Aya 57

17 : 57

Aya 57 of الإسرَاء (17 : 57). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الإسرَاء Aya 111
Sura · الإسرَاء
Kiswahili · Barawani
17 : 57

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ يَبۡتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ ٱلۡوَسِيلَةَ أَيُّهُمۡ أَقۡرَبُ وَيَرۡجُونَ رَحۡمَتَهُۥ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُۥٓۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحۡذُورٗا

Hao wanao waomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi - hata miongoni mwao walio karibu mno - na wanataraji rehema zake na wanaikhofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhari nayo.

Explanation & meanings · 1
  1. Na hakika hawa viumbe wanao waomba wale wanao waabudu, wao wenyewe wanamuabudu Mwenyezi Mungu, na wanaomba wapate daraja na cheo kwake kwa ut'iifu, na wana pupa ya kutaka wawe karibu zaidi na Mwenyezi Mungu, na wanatumaini kupata kwake rehema, na wanaikhofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mwenyezi Mungu inatakikana kutahadhari nayo na kuiogopa!