Skip to content
الإسرَاء /

Aya 23

17 : 23

Aya 23 of الإسرَاء (17 : 23). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الإسرَاء Aya 111
Sura · الإسرَاء
Kiswahili · Barawani
17 : 23

۞ وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّآ إِيَّاهُ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنًاۚ إِمَّا يَبۡلُغَنَّ عِندَكَ ٱلۡكِبَرَ أَحَدُهُمَآ أَوۡ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَآ أُفّٖ وَلَا تَنۡهَرۡهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوۡلٗا كَرِيمٗا

Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima.

Explanation & meanings · 1
  1. Na Mola wako Mlezi amehukumu kuwa msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye. Na pia muwafanyie wema kwa ukamilifu wazazi wenu wawili. Na hao, au mmoja wao, wakifikilia kwako hali ya unyonge na mwisho wa umri wao, basi lisikutoke tamko la kuchoka nao au kuudhika kwa yanayo kupata kutokana nao. Wala usiwahamakie. Na nena nao maneno mazuri, laini, yenye kuwaonyesha ihsani na kuwahishimu.