Skip to content
البَقَرَة /

Aya 11

2 : 11

Aya 11 of البَقَرَة (2 : 11). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 11

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ لَا تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ قَالُوٓاْ إِنَّمَا نَحۡنُ مُصۡلِحُونَ

Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji.

Explanation & meanings · 1
  1. Na pindi mmojawapo wa walio ongoka akiwaambia hawa wanaafiki: "Msifanye uharibifu katika nchi kwa kuipinga Njia ya Mwenyezi Mungu, na kueneza fitna, na kuwasha moto wa vita," wao hujitoa makosani mwa uharibifu, na husema: "Kee sisi ndio tunao tengeneza." Na hayo ni kwa kuwa ghururi yao imepita mpaka. Huu ndio mwendo wa kila mharibifu, khabithi mwenye ghururi. Yeye hudai kuwa ule uharibifu wake ndio matengenezo na maendeleo.