Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa, au akafanya ukuhani au akafanyiwa, au akaroga au akarogewa
Imepokewa kutoka kwa Imran bin Huswain - Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-
"Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa, au akafanya ukuhani au akafanyiwa, au akaroga au akarogewa, na atakayefunga fundo lolote, na atakayemuendea kuhani na akamsadikisha kwa yale ayasemayo atakuwa amekufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammadi Rehema na amani ziwe juu yake".
«لَيْسَ مِنَّا مَنْ تَطَيَّرَ أَوْ تُطُيِّرَ لَهُ، أَوْ تَكَهَّنَ أَوْ تُكُهِّنَ لَهُ، أَوْ سَحَرَ أَوْ سُحِرَ لَهُ، وَمَنْ عَقَدَ عُقْدَةً، وَمَنْ أَتَى كَاهِنًا فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ».
Katoa onyo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa atakayefanya baadhi ya matendo katika umma wake kwa kauli yake: "Si miongoni mwetu" Miongoni mwayo: La kwanza: "Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa" Na asili ya hili: Ni kumuachia ndege wakati wa kuanza kazi kama safari au biashara au mengineyo, akiruka upande wa kulia anajipa matumaini na anaendelea na analolitaka, na akirukia upande wa kushoto anaamini ni mkosi anaacha alichokikusudia, haifai kufanya hivi au kumlipa mwenye kumfanyia hivi, na inaingia hapa kupiga bao kwa kitu chochote sawa sawa chenye kusikika au kuonekana, kama ndege au wanyama au wenye ulemavu au namba au siku au mengineyo. La pili: "Atakayefanya ukuhani au akafanyiwa" Atakayedai kujua elimu ya yaliyofichikana kwa kutumia nyota na vinginevyo, au akaja kwa anayedai kujua elimu ya yaliyofichikana kama kuhani na mfano wake, akamsadikisha kwa yale ayasemayo kwa kudai kwake kujua elimu ya ghaibu, basi atakuwa kakufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake. La tatu: "Atakayeroga au akarogewa" Naye ni yule atakayefanya uchawi yeye mwenyewe, au akampa kazi atakayemfanyia uchawi; ili amnufaishe yeyote au amdhuru, au akafunga fundo lolote kwa kufunga na nyuzi na kuzirogea kwa kusoma kinga za kishirikina zilizoharamishwa na akazipuliza.
...:
Uwajibu wa kumtegemea Allah na kuamini hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake, na kuharamishwa kwa imani za mikosi na nuksi na uchawi na ukuhani, au kuwauliza wenye mambo hayo.
Kudai kujua elimu ya ghaibu ni katika shirki inayopingana na tauhidi.
Uharamu wa kuwasadikisha makuhani na kuwaendea, na vinaingia hapa kusoma viganja na kusoma yaliyoandikwa kwenye vikombe na kutazamia nyota na, hata kama ni kwa kutaka kujua.
Zaidi (11)
مسند البزار = البحر الزخار (9/ 52) (3578).
شرح السنة للبغوي (12/ 182).
مجموع الفتاوى (35/ 173).
القول المفيد على كتاب التوحيد.
لابن عثيمين (1/ 543).
التمهيد لشرح كتاب التوحيد.
لصالح آل الشيخ (ص315).
الجديد في شرح كتاب التوحيد.
لمحمد القرعاوي (ص242).
الملخص في شرح كتاب التوحيد.
لصالح الفوزان (ص217).
Imenukuliwa katika vitabu
7 Vitabu- Kitabu cha Tauheed {upwekeshaji}كتاب التوحيد للشيخ محمد بن عبد الوهاب"Atakayemuendea kuhani na akamsadikisha kwa yale anayoyasema basi atakuwa amekufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammadi Sala na Amani ziwe juu yake"
- Kitabu cha Tauheed {upwekeshaji}كتاب التوحيد للشيخ محمد بن عبد الوهاب"Si miongoni mwetu mwenye kuitakidi mikosi kupitia ndege, au mwenye kuwa kuhani au akafanyiwa ukuhani, au akafanya uchawi, au akataka afanyiwe uchawi, na atakaye mwendea kuhani na akamsadikisha ayasemayo, basi huyo kayakufuru aliyokuja nayo
Zaidi (5)
- حكم السحر والكهانة(من أتى كاهناً فصدّقه بما يقول فقد كفر بما أنزل على محمد -صلى الله عليه وسلم- )
- حكم السحر والكهانة(من أتى كاهناً فصدقه بما يقول فقد كفر بما أنزل على محمد -صلى الله عليه وسلم- )،
- حكم السحر والكهانة(من أتى كاهناً فصدقه بما يقول فقد كفر بما أنزل على محمد -صلى الله عليه وسلم- )،
- عقيدة الأئمة الأربعة«لَيْسَ مِنَّا مَنْ تَطَيَّرَ أَوْ تُطِيِّرَ لَهُ، أَوْ تَكَهَّنَ أَوْ تُكُهِّنَ لَهُ، أَوْ سَحَرَ أَوْ سُحِرَ لَهُ»،
- مطوية الرقيةالرقية الشرعية - 1" ليس منّا مَن تطيّر أو تُطير له، أو تكهّن أو تُكهّن له، أو سَحر أو سُحر له، ومن أتى كاهناً فصدقه بما يقول فقد كفر بما أنزل على محمد ".