Skip to content
Orodha ya Sura /

الانشِقَاق

الانشِقَاق is chapter 84 of the Quran and has 25 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

25 Aya Sura Na. 84
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتۡ

Itapo chanika mbingu!

Explanation & meanings · 1
  1. Mbingu itapo chanika, ikaamrishwa iondoke,

وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ

Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza!

Explanation & meanings · 1
  1. Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi na ikamt'ii, na ndio maelekeo yake isikie na kut'ii,

وَإِذَا ٱلۡأَرۡضُ مُدَّتۡ

Na ardhi itakapo tanuliwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Na ardhi ikazidi upana wake kwa kulazwa milima na kuondolewa kifusi chake,

وَأَلۡقَتۡ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتۡ

Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu!

Explanation & meanings · 1
  1. Na ardhi ikatoa nje maiti na khazina ziliyo kuwamo ndani yake, na ikaachana navyo vyote hivyo,

وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ

Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza!

Explanation & meanings · 1
  1. Na ikamwelekea Mola wake Mlezi kwa kuzidi kutanuka kwake na kutoa vilio kuwemo ndani yake na kuachana navyo, na hayo ni haki yake kuwa. Yakitokea yote hayo yaliyo tangulia kusimuliwa basi kila mtu atapata malipo ya vitendo vyake.