Skip to content
Orodha ya Sura /

البُرُوج

البُرُوج is chapter 85 of the Quran and has 22 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

22 Aya Sura Na. 85
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡبُرُوجِ

Naapa kwa mbingu yenye Buruji!

Explanation & meanings · 1
  1. Naapa kwa mbingu yenye Buruj au Manaazil, njia au vituo ambavyo nyota hupitia katika nyendo zake, Buruuj au Manaazil ndio huu mkusanyiko wa nyota unao onekana kwa sura namna mbali mbali mbinguni. Hizo Buruuj zimegawika sehemu kumi na mbili ambazo ardhi inazipitia inapo lizunguka jua.

وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡمَوۡعُودِ

Na kwa siku iliyo ahidiwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa Siku iliyo ahidiwa kuwa ndiyo Siku ya Hisabu na Malipo,

وَشَاهِدٖ وَمَشۡهُودٖ

Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa viumbe watao hudhuria Siku hiyo wakaona vitisho na ajabu zitakazo kuwepo,

قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ

Wameangamizwa watu wa makhandaki.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika Mwenyezi Mungu amewalaani watu walio chimba khandaki katika ardhi,

ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ

Yenye moto wenye kuni nyingi!

Explanation & meanings · 1
  1. Wakawasha moto kuwatumbukiza ndani yake Waumini ili kuwatesa,