Skip to content
Orodha ya Sura /

المُطَففين

المُطَففين is chapter 83 of the Quran and has 36 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

36 Aya Sura Na. 83
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَيۡلٞ لِّلۡمُطَفِّفِينَ

Ole wao hao wapunjao!

Explanation & meanings · 1
  1. Wataangamia wanao punja,

ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكۡتَالُواْ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسۡتَوۡفُونَ

Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.

Explanation & meanings · 1
  1. Ambao wakijipimia wenyewe kwa watu hujitwalia ya kutosha na kuzidi,

وَإِذَا كَالُوهُمۡ أَو وَّزَنُوهُمۡ يُخۡسِرُونَ

Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.

Explanation & meanings · 1
  1. Na wakiwapimia watu kwa vipimo au mizani huwapunguzia haki yao wanayo stahiki, kwa dhulma!

أَلَا يَظُنُّ أُوْلَٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبۡعُوثُونَ

Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa .

Explanation & meanings · 1
  1. Hivyo haiwapitikii katika akili zao hawa wanao punja wenzao kwamba watakuja fufuliwa,

لِيَوۡمٍ عَظِيمٖ

Katika Siku iliyo kuu!

Explanation & meanings · 1
  1. Katika siku ya vitisho vikuu?