Skip to content
Orodha ya Sura /

الذَّاريَات

الذَّاريَات is chapter 51 of the Quran and has 60 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

60 Aya Sura Na. 51
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلذَّٰرِيَٰتِ ذَرۡوٗا

Naapa kwa pepo zinazo tawanya!

Explanation & meanings · 1
  1. Ninaapa kwa pepo zinazo timua mawingu, zikayasukuma kwa nguvu, huku zikibeba mizigo mizito ya maji, zikawa zinakwenda kwa wepesi kwa amri ya Mwenyezi Mungu, zikawa zinagawanya riziki kwa ampendaye Mwenyezi Mungu.

فَٱلۡحَٰمِلَٰتِ وِقۡرٗا

Na zinazo beba mizigo!

Explanation & meanings · 1
  1. Huku zikibeba mizigo mizito ya maji.

فَٱلۡجَٰرِيَٰتِ يُسۡرٗا

Na zinazo kwenda kwa wepesi.

Explanation & meanings · 1
  1. Zikawa zinakwenda kwa wepesi kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

فَٱلۡمُقَسِّمَٰتِ أَمۡرًا

Na zinazo gawanya kwa amri!

Explanation & meanings · 1
  1. Zikawa zinagawanya riziki kwa ampendaye Mwenyezi Mungu.

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٞ

Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli!

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika hayo mnayo ahidiwa, nayo ya kufufuliwa na mengineyo, ni hakika ya kweli itakayo tokea.