51 : 44
فَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ وَهُمۡ يَنظُرُونَ
Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona.
Explanation & meanings · 1
- Na katika kisa cha Thamudi ipo Ishara. Walipo ambiwa: Stareheni katika majumba yenu kwa muda maalumu. Wakajivuna na wakatakabari wasifuate amri ya Mola wao Mlezi. Basi radi ikawaangamiza nao wanaiona kwa macho yao inavyo tokea.