Skip to content
Orodha ya Sura /

قٓ

قٓ is chapter 50 of the Quran and has 45 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

45 Aya Sura Na. 50
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

قٓۚ وَٱلۡقُرۡءَانِ ٱلۡمَجِيدِ

Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu!

Explanation & meanings · 1
  1. Qaaf. Hii ni harufi katika harufi za alifbete iliyo fungulia Sura hii kama ilivyo ada ya Qur'ani katika kufungulia Sura kadhaa wa kadhaa kwa harufi kama hii, ili kuwakabili makafiri kama wanaweza kuleta mfano wake, na pia kuwazindua watu wasikilize yanayo somwa. Ninaapa kwa Qur'ani yenye ubora, na utukufu, na hishima kwamba hakika Sisi tumekutuma wewe, ewe Muhammad, ili uwaonye watu kwa hii.

بَلۡ عَجِبُوٓاْ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٞ مِّنۡهُمۡ فَقَالَ ٱلۡكَٰفِرُونَ هَٰذَا شَيۡءٌ عَجِيبٌ

Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema makafiri: Hili ni jambo la ajabu!

Explanation & meanings · 1
  1. Bali walistaajabu kutokea Mtume miongoni mwa jinsi yao akiwaonya kuwa watafufuliwa. Makafiri wakasema: Jambo hili hatulijui, na la ajabu!

أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗاۖ ذَٰلِكَ رَجۡعُۢ بَعِيدٞ

Ati tukifa na tukawa udongo? Kurejea huko kuko mbali!

Explanation & meanings · 1
  1. Ati baada ya kwisha kufa na tukawa udongo, tutafufuliwa tena? Huko kufufuliwa baada ya kufa ni marejeo yaliyo mbali, hayawi.

قَدۡ عَلِمۡنَا مَا تَنقُصُ ٱلۡأَرۡضُ مِنۡهُمۡۖ وَعِندَنَا كِتَٰبٌ حَفِيظُۢ

Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinacho punguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinacho hifadhi yote.

Explanation & meanings · 1
  1. Sisi hakika tunajua vipi ardhi inavyo vimeza viwiliwili vyao baada ya kufa. Na Sisi tunacho Kitabu kinacho dhibiti na kuhifadhi kila kitu hata kidogo.

بَلۡ كَذَّبُواْ بِٱلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمۡ فَهُمۡ فِيٓ أَمۡرٖ مَّرِيجٍ

Lakini waliikanusha Haki ilipo wajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mkorogo.

Explanation & meanings · 1
  1. Wao hawayazingatii aliyo kuja nayo Mtume, bali walimkadhibisha mara tu bila ya kuzingatia na kufikiri. Basi wao wamo katika hali ya kubabaika, hawana utulivu.