Skip to content
Orodha ya Sura /

الطُّور

الطُّور is chapter 52 of the Quran and has 49 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

49 Aya Sura Na. 52
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلطُّورِ

Naapa kwa mlima wa T'ur!

Explanation & meanings · 1
  1. Ninaapa kwa mlima wa T'ur ulioko katika Sinai. Kwenye mlima huo ndio Nabii Musa a.s. alisemezwa.

وَكِتَٰبٖ مَّسۡطُورٖ

Na Kitabu kilicho andikwa .

Explanation & meanings · 1
  1. Ninaapa kwa mlima wa T'ur ulioko katika Sinai. Kwenye mlima huo ndio Nabii Musa a.s.

فِي رَقّٖ مَّنشُورٖ

Katika ngozi iliyo kunjuliwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Kilicho andikwa katika kurasa zilio nyepesi kuzisoma,

وَٱلۡبَيۡتِ ٱلۡمَعۡمُورِ

Na kwa Nyumba iliyo jengwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa Nyumba iliyo jengwa kwa sababu ya wenye kuizunguka kwa ibada na wenye kusimama na kurukuu na kusujudu kwa Swala,

وَٱلسَّقۡفِ ٱلۡمَرۡفُوعِ

Na kwa dari iliyo nyanyuliwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Na naapa kwa mbingu iliyo nyanyuliwa bila ya nguzo, na bahari iliyo jaa.