Skip to content
Orodha ya Sura /

الدُّخان

الدُّخان is chapter 44 of the Quran and has 59 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

59 Aya Sura Na. 44
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

حمٓ

H'a Mim .

Explanation & meanings · 1
  1. H'a Mim. Imeanzia Sura hii kwa baadhi ya harufi za kutamkwa kama ilivyo ada ya Qur'ani katika kufungulia Sura nyingi kwa harufi kama hizi.

وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ

Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha!

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu anaapa kwa Qur'ani yenye kuweka wazi Dini ya Haki, yenye kuwabainishia watu yaliyo na maslaha ya dunia yao na Akhera yao, ili kujuulisha utukufu wa cheo chake.

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةٖ مُّبَٰرَكَةٍۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ

Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika Sisi tumeanza kuiteremsha Qur'ani katika usiku ulio jaa kheri, wenye baraka nyingi, kwani ni mwendo wetu kuonya kwa kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu.

فِيهَا يُفۡرَقُ كُلُّ أَمۡرٍ حَكِيمٍ

Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima!

Explanation & meanings · 1
  1. Katika usiku huu wenye baraka hupambanuliwa baina ya mambo yote yenye hikima, na Qur'ani ndio kilele cha hikima, na ndio pambanuo baina ya kweli na uwongo. Na kwa hivyo ndio ikateremshwa katika usiku huo.

أَمۡرٗا مِّنۡ عِندِنَآۚ إِنَّا كُنَّا مُرۡسِلِينَ

Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.

Explanation & meanings · 1
  1. Nakusudia kwa jambo hili, yaani jambo kuu lenye kutoka kwetu kama ilivyo kwisha pita hukumu ya mpango wetu. Kwani ni shani yetu kutuma Mitume kwa Vitabu ili kuwafikishia waja wetu.