Skip to content
Orodha ya Sura /

الجاثِية

الجاثِية is chapter 45 of the Quran and has 37 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

37 Aya Sura Na. 45
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

حمٓ

H'a Mim .

Explanation & meanings · 1
  1. H'a Mim. Hizi ni harufi mbili katika harufi za kutamkwa, zimeanzia Sura hii kama ada ya Sura nyingi katika Qur'ani ambazo zimeanzia kwa harufi kama hivi ili kuashiria kuwa washirikina wameshindwa kuleta mfano wake, ijapo kuwa hii Qur'ani imeundwa kwa harufi hizi hizi wanazo zitumia katika maneno yao.

تَنزِيلُ ٱلۡكِتَٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ

Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

Explanation & meanings · 1
  1. Huu mteremsho wa Qur'ani umetokana na Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Asiye shindika, Mwenye hikima katika kupanga kwake na kuendesha kwake.

إِنَّ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ لَأٓيَٰتٖ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ

Hakika katika mbingu na ardhi ziko Ishara kwa Waumini.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi ni katika ufundi wa namna ya pekee wa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka ni dalili zenye nguvu kabisa katika Ungu wake na Upweke wake, ambao wanauamini wenye kumsadiki Mwenyezi Mungu kwa maumbile yao yaliyo sawa.

وَفِي خَلۡقِكُمۡ وَمَا يَبُثُّ مِن دَآبَّةٍ ءَايَٰتٞ لِّقَوۡمٖ يُوقِنُونَ

Na katika umbo lenu na katika wanyama alio watawanya zimo Ishara kwa watu wenye yakini.

Explanation & meanings · 1
  1. Na vile Mwenyezi Mungu kukuumbeni nyinyi, enyi watu, kama mlivyo, mna sura nzuri, na umbo la peke yenu, na mnavyo khitalifiana baina ya wanaadamu na wanyama na mkaenezwa ulimwenguni, na manufaa mbali mbali, bila ya shaka ni Ishara zenye nguvu na ziwazi kwa watu wanao tafuta yakini ya mambo yao kwa kuzingatia na kufikiri.

وَٱخۡتِلَٰفِ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ وَمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مِن رِّزۡقٖ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَا وَتَصۡرِيفِ ٱلرِّيَٰحِ ءَايَٰتٞ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ

Na kupishana usiku na mchana, na riziki anayo iteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake, na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili.

Explanation & meanings · 1
  1. Na katika kukhitalifiana usiku na mchana, kwa urefu na ufupi, na mwangaza na giza, na kupeana zamu kwa nidhamu iliyo thibiti, na katika mvua anayo iteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, akaihuisha ardhi kwa mimea baada ya kufa kwake kwa ukame, na kuziendesha pepo pande mbali mbali nazo zinakhitalifiana kwa ubaridi na joto, na nguvu na udhaifu, ni alama zilizo wazi za kuonyesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye kufikiri kwa akili zao, wakafikilia yakini yao.