44 : 19
وَأَن لَّا تَعۡلُواْ عَلَى ٱللَّهِۖ إِنِّيٓ ءَاتِيكُم بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ
Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi.
Explanation & meanings · 1
- Wala msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu kwa kumkadhibisha Mtume wake, kwani mimi nakuleteeni muujiza ulio wazi wa kubainisha ukweli wa Unabii wangu na Utume wangu.