Skip to content

Kusibaki katika shingo la mnyama bangili za shaba au kengele isipokuwa (ahakikishe) zimekatwa

Kutoka kwa Abuu Bashiri Radhi za Allah ziwe juu yake:

Yakwamba yeye alikuwa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya safari zake, anasema: Akatuma mjumbe Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na watu wakiwa mahali pao pa kulala: "Kusibaki katika shingo la mnyama bangili za shaba au kengele isipokuwa (ahakikishe) zimekatwa".

أَنَّهُ كَانَ مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي بَعْضِ أَسْفَارِهِ، قَالَ: فَأَرْسَلَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَسُولًا -وَالنَّاسُ فِي مَبِيتِهِمْ-: «لَا يَبْقَيَنَّ فِي رَقَبَةِ بَعِيرٍ قِلَادَةٌ مِنْ وَتَرٍ أَوْ قِلَادَةٌ إِلَّا قُطِعَتْ».

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Ufafanuzi

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya safari zake, na watu wakiwa mahali pao pa kulala wanapopumzikia katika vipandwa vyao na mahema yao, akamtuma mtu kwenda kwa watu akawaamrishe wakate vikamba vinavyotundikwa kwa wanyama sawa sawa ziwe zimetokana na kamba ya upinde -kamba ya upinde, au kinginecho kama kengele au kiatu, na hii ni kwa sababu walikuwa wakitundika kwa kuogopa kijicho, wakaamrishwa kuvikata; kwa sababu havizuii kwao chochote, nakuwa manufaa na madhara yako mkononi mwa Allah peke yake asiye na mshirika.

Maana ya Maneno

وتر: مفرد أوتار، وهو ما يشد به القوس كانت العرب تعلقه تتقي به العين.

قلادة: ما يعلق في رقبة البعير وغيره، كالجرس والنعل، بنية دفع العين.

Katika Faida za Hadithi

Uharamu wa kutundika makamba na kengele kwa ajili ya kuleta manufaa au kuzuia madhara; kwani hilo ni katika ushirikina.

Kufunga kengele isiyoambatana na itikadi, kwa ajili ya urembo, au kuongozea mnyama au kumfungia haina tatizo.

Uwajibu wa kukemea uovu kulingana na uwezo.

Uwajibu wa moyo kuambatana na Allah peke yake asiye na mshirika.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (4/ 59) (3005).

Swahiih Muslim (3/ 1672) (2115).

Zaidi (6)

القول المفيد على كتاب التوحيد.

لابن عثيمين (1/ 179).

الملخص في شرح كتاب التوحيد.

لصالح الفوزان (ص77).

الجديد في شرح كتاب التوحيد.

لمحمد القرعاوي (ص89).