عربي - Arabic English Qafár af - Afar Afrikaans - Afrikanns Akan Shqip - Albanian አማርኛ - Amharic Հայերեն - Armenian অসমীয়া - Assamese Azərbaycanca - Azerbaijani Bamanankan - Bambara Bassa Bemba বাংলা - Bengali Bosanski - Bosnian Български - Bulgarian မြန်မာဘာသာ - Burmese Bisaya - Cebuano Cham Нохчий - Chechen chiCheŵa - Chewa 中文 - Chinese Адыгэбзэ - Circassian Hrvatski - Croatian Česky - Czech Dagbani Dansk - Danish فارسی دری - Dari Dendi ދިވެހި ބަސް - Dhivehi Nederlands - Dutch إستوني - Estonian Suomi - Finnish Français - French Fulfulde - Fula ქართული - Georgian Deutsch - German Ελληνικά - Greek ગુજરાતી - Gujrati Kreyòl ayisyen - Haitian Creole Hausa हिन्दी - Hindi Magyar - Hungarian Igbo Indonesia - Indonesian Italiano - Italian 日本語 - Japanese Jóola - Jola ಕನ್ನಡ - Kannada Қазақша - Kazakh ភាសាខ្មែរ - Khmer Kikuyu Ikinyarwanda - Kinyarwanda Ikirundi - Kirundi 한국어 - Korean كوردی سۆرانی - kurdish كوردي kurmancî - Kurmanji Kyrgyz ລາວ - Lao latviešu - Latvian Lingala lietuvių - Lithuanian Luganda Македонски - Macedonian Maguindanaon Malagasy - Malagasy Bahasa Melayu - Malay മലയാളം - Malayalam Mandinka मराठी - Marathi Mõõré - Moore नेपाली - Nepali أنكو - NKo Norwegian ଓଡ଼ିଆ - Odia oromoo - Oromo پښتو - Pashto فارسی - Persian Polski - Polish Portuguese ਪੰਜਾਬੀ - Punjabi Română - Romanian Русский - Russian Српски - Serbian Shona සිංහල - Sinhala Slovenščina - Slovenian Soomaaliga - Somali Soninke Sesotho - Sotho Español - Spanish Kiswahili - Swahili Svenska - Swedish Tagalog Тоҷикӣ - Tajik தமிழ் - Tamil తెలుగు - Telugu ไทย - Thai ትግረኛ - Tigrinya Türkçe - Turkish Ukrainian اردو - Urdu ئۇيغۇرچە - Uyghur Ўзбек - Uzbek Việt Nam - Vietnamese Wolof Yao Yorùbá - Yoruba Zarma زولو - Zulu
839 Hadithi
Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii
Makundi
Daraja la hadithi
Imesimuliwa katika
Msimulizi
Onyesha wasimulizi wote (23)
"Mambo manne yatakayekuwa kwake basi atakuwa mnafiki, ana akiwa na jambo moja miongoni mwa hayo basi atakuwa na tabia ya unafiki mpaka aiache: Yule anayesimulia akasema uongo, na akiahidi hatimizi, na akigombana hupita mipaka, na akiingia makubaliano hufanya hiyana".
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Muslim
Shetani humjia mmoja wenu na akamwambia: Ni nani aliumba kitu fulani? Mpaka anafikia kusema ni nani alimuumba Mola wako? Basi ikiwa atafikia kuuliza hivyo basi na ajikinge kwa Mwenyezi Mungu na awache kuuliza maswali hayo."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Atakayeiapia amana basi huyo si miongoni mwetu".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud na Ahmad
Alisema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Muadhi Ibn Jabal, alipomtuma kwenda Yemen: "Hakika wewe utaiendea jamii ya watu wa kitabu (Mayahudi na Wakristo), utakapowajia basi waite kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Ikiwa watakutii kwa hilo, basi waeleze kuwa Mwenyezi Mungu amewalazimisha juu yao swala tano katika kila usiku na mchana, ikiwa watakutii kwa hilo, basi waeleze kuwa Mwenyezi Mungu amewalazimisha juu yao zaka, huchukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kurudishwa kwa mafukara wao, ikiwa watakutii kwa hilo, basi jiepushe na mali zao za thamani, na ogopa maombi ya mwenye kudhulumiwa, kwani maombi hayo hayana baina yake na Mwenyezi Mungu kizuizi".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri: Kutiana doa katika nasaba (ukoo), na kulia kwa kumuomboleza maiti".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu muumini kwa jema alilofanya, huandikiwa thawabu za wema wake hapa Duniani na hulipwa thawabu hizo huko Akhera Ama kafiri hulishwa kwa mema aliyoyafanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hapa duniani, mpaka akifika Akhera anakuwa hana jema lolote ambalo atalipwa nalo."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Umejengwa uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mja wake na Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba tukufu, na kufunga ramadhani".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Mfano wa mtu mnafiki, ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga baina ya makundi mawili ya Mbuzi, wakati mwingine huwa na kundi hili na wakati mwingine huwa na kundi lile."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim