Skip to content
Orodha ya Sura /

النَّجم

النَّجم is chapter 53 of the Quran and has 62 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

62 Aya Sura Na. 53
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلنَّجۡمِ إِذَا هَوَىٰ

Naapa kwa nyota inapo tua!

Explanation & meanings · 1
  1. Ninaapa kwa nyota inapo tua kwa kuchwa, ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu.

مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمۡ وَمَا غَوَىٰ

Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea.

Explanation & meanings · 1
  1. ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu.

وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلۡهَوَىٰٓ

Wala hatamki kwa matamanio.

Explanation & meanings · 1
  1. Wala halitoki katika anayo yatamka ya Qur'ani kwa mapendo ya nafsi yake.

إِنۡ هُوَ إِلَّا وَحۡيٞ يُوحَىٰ

Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa; .

Explanation & meanings · 1
  1. Hii Qur'ani anayo itamka si chochote ila ni Wahyi (Ufunuo) ulio toka kwa Mwenyezi Mungu anamfunulia yeye.

عَلَّمَهُۥ شَدِيدُ ٱلۡقُوَىٰ

Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu!

Explanation & meanings · 1
  1. Aliye mfundisha ufunuo huu ni mwenye nguvu nyingi.