Skip to content
Orodha ya Sura /

القَمَر

القَمَر is chapter 54 of the Quran and has 55 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

55 Aya Sura Na. 54
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱقۡتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلۡقَمَرُ

Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!

Explanation & meanings · 1
  1. Kiyama kimekaribia na mwezi utapasuka hapana hivi wala hivi.

وَإِن يَرَوۡاْ ءَايَةٗ يُعۡرِضُواْ وَيَقُولُواْ سِحۡرٞ مُّسۡتَمِرّٞ

Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.

Explanation & meanings · 1
  1. Na makafiri wakiona Ishara, yaani muujiza mkubwa, wao hupuuza wakaacha kuuamini. Bali husema: Huu ni uchawi wa daima unaendelea!

وَكَذَّبُواْ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَكُلُّ أَمۡرٖ مُّسۡتَقِرّٞ

Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti.

Explanation & meanings · 1
  1. Na wamewakanusha Mitume na wakafuata yaliyo zainishwa na matamanio yao. Na kila jambo huishia mwisho wake linapo tulia na kuthibiti.

وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّنَ ٱلۡأَنۢبَآءِ مَا فِيهِ مُزۡدَجَرٌ

Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio.

Explanation & meanings · 1
  1. Na ninaapa kuwa zimewajia makafiri khabari za mataifa yaliyo tangulia zenye ukweli wa uumbaji ambazo zina mikemeo ya kutosha.

حِكۡمَةُۢ بَٰلِغَةٞۖ فَمَا تُغۡنِ ٱلنُّذُرُ

Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu!

Explanation & meanings · 1
  1. Haya yaliyo wajia ni hikima kubwa na lengo la kufikia mbali. Lakini maonyo yataleta faida gani kwa wanao zipinga hikima hizo?