53 : 52
وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ هُمۡ أَظۡلَمَ وَأَطۡغَىٰ
Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi;
Explanation & meanings · 1
- Na aliwaangamiza kaumu ya Nuhu kabla ya kuwaangamiza A'di na Thamudi. Hakika hao walikuwa wamekithiri kudhulumu, na wamezidi kwa uasi kuliko A'di na Thamudi.