Skip to content

Yeyote atakaye kujieni hali yakuwa mmekubaliana kumfanya kiongozi mtu mmoja, akataka kupasua nguvu yenu, Au ausambaratishe umoja wenu, basi muuweni

Imepokewa kutoka kwa Farja -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema:

"Yeyote atakaye kujieni hali yakuwa mmekubaliana kumfanya kiongozi mtu mmoja, akataka kupasua nguvu yenu, Au ausambaratishe umoja wenu, basi muuweni".

«مَنْ أَتَاكُمْ وَأَمْرُكُمْ جَمِيعٌ عَلَى رَجُلٍ وَاحِدٍ، يُرِيدُ أَنْ يَشُقَّ عَصَاكُمْ، أَوْ يُفَرِّقَ جَمَاعَتَكُمْ، فَاقْتُلُوهُ».

Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa waislamu watakapokubaliana juu ya kiongozi mmoja, na mshikamano mmoja, kisha akaja anayetaka kumpokonya madaraka, au akataka kuwasambaratisha waislamu kuwafanya kuwa makundi makundi, ni lazima wamzuie na wampige vita, kwa kuzuia shari yake, na kwa kuhifadhi damu za waislamu.

Maana ya Maneno

وأمركم جميع: كلمتكم مجتمعة على إمام واحد، وأنتم يد واحدة.

يشق عصاكم: أصل العصا الاجتماع والائتلاف، والمراد هنا أنه يريد تفريق جماعتكم التي اجتمعت على إمام واحد.

Katika Faida za Hadithi

Ulazima wa kumtii kiongozi anayesimamia mambo ya waislamu, katika mambo yasiyokuwa maasi, na uharamu wa kujitoa dhidi yake.

Atakayejitoa kwa kiongozi wa waislamu na umoja wao, basi ni wajibu kumpiga vita vyovyote vile itakavyokuwa nafasi yake ya cheo au ukoo.

Himizo la kuwa wamoja na kutofarakana na kuhitilafiana.

Rejea

Swahiih Muslim (3/ 1480) (1852).

Zaidi (8)

منحة العلام في شرح بلوغ المرام.

لعبد الله الفوزان (8/ 349).

توضيح الأحكام شرح بلوغ المرام.

للبسام (6/ 329).

فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام.

لابن عثيمين (5/ 302).

المفاتيح في شرح المصابيح.

الحسين المُظْهِري (4/ 295).