Mimi nina mama mzazi ambaye anafikia umri wa miaka sitini na tano, na yeye katika kipindi cha miaka kumi na tisa hajapata mtoto, na hivi sasa ana kipindi cha miaka mitatu akiwa na ugonjwa wa kutokwa na damu, -na inavyoonekana nikuwa- maradhi hayo yalimpata katika wakati huo vile vile anakabiliwa na ibada ya swaumu, je ni nini nasaha zenu kwake, na je, nini atakachotakiwa kufanya?
السؤال
Swali la 1:
Mimi nina mama mzazi ambaye anafikia umri wa miaka sitini na tano, na yeye katika kipindi cha miaka kumi na tisa hajapata mtoto, na hivi sasa ana kipindi cha miaka mitatu akiwa na ugonjwa wa kutokwa na damu, -na inavyoonekana nikuwa- maradhi hayo yalimpata katika wakati huo vile vile anakabiliwa na ibada ya swaumu, je ni nini nasaha zenu kwake, na je, nini atakachotakiwa kufanya?
س33: لي والدةٌ تبلغ من العمر خمسةً وستّين عامًا، ولها مدة تسع عشرة سنةً وهي لم تأت بأطفالٍ، والآن معها نزيف دمٍ، لها مدة ثلاث سنواتٍ، وهو مرضٌ -يبدو- أتاها في تلكم الفترة، ولأنها ستستقبل الصّيام، فكيف تنصحونها؟ وكيف يتصرف مثلها؟
الجواب
Jawabu la 1:
Hukumu ya mfano wa mwanamke kama huyu aliyefikwa na ugonjwa wa kutokwa na damu: Anatakiwa aache kuswali na kufunga katika kipindi cha desturi yake iliyotangulia kabla ya kufikwa na ugonjwa huu. Hivyo basi iwapo ilikuwa kawaida yake anapata hedhi katika mwanzo wa kila mwezi kwa muda wa siku sita kwa mfano, basi atakaa katika mwanzo wa kila mwezi kwa muda wa siku sita na hali ya kuwa haswali wala hafungi, na zitakapoisha siku hizo basi ataoga na ataswali na atafunga.
Na namna ya swala ya mwanamke kama huyu na mfano wake: Ataosha tupu yake kwa ukamilifu, halafu ataifunga na atatawadha, na atakuwa akifanya hivyo baada ya kuingia wakati wa kila swala ya faradhi, na atafanya hivyo hivyo atakapokuwa anataka kuswali swala za suna zisizokuwa faradhi.
Na katika hali kama hii, na kutokana na tabu anazopitia, itakuwa inajuzu kwake kukusanya swala ya Adhuhuri na Laasiri, na swala ya Magharibi na Ishaa: Kwa kufanya kwake hivi ataswali swala mbili kwa mara moja; Yaani swala ya Adhuhuri na Alasiri.
Na twahara moja pia kwa ajili ya swala mbili: Yaani swala ya Magharibi na Ishaa, na Alfajiri itakuwa pekee. Hivyo basi badala ya kuswali mara tano ataswali mara tatu tu.
Na hapa nitarudia maelezo mara ya pili, ninasema: Pindi atakapotaka kujitwaharisha ataosha tupu yake, na ataifunga kwa kitambaa au mfano wa kitambaa, ili ipungue ile hali ya kutoka damu. Kisha atatawadha, na ataswali Adhuhuri rakaa nne na Alasiri rakaa nne. Na Magharibi rakaa tatu na Ishaa rakaa nne, na Alfajiri rakaa mbili, kwa maana kwamba asipunguze rakaa hizo kama wanavyodhania baadhi ya watu wasiokuwa na elimu na maarifa.
Lakini inajuzu kwake kukusanya kati ya swala ya Adhuhuri na Alasiri, na kati ya swala ya Magharibi na Ishaa, ima kwa kutanguliza au kwa kuchelewesha, na ikiwa atataka kuswali swala ya sunna kwa udhu huo huo aliyoswalia swala hizo za faradhi, hapana ubaya kufanya hivyo.
ﺟ33: مثل هذه المرأة التي أصابها نزيف الدم حكمها: أن تترك الصلاة والصوم مدة عادتها السابقة قبل هذا الحدث الذي أصابها، فإذا كان من عادتها أن الحيض يأتيها من أول كلّ شهرٍ لمدة ستة أيامٍ مثلًا، فإنها تجلس من أول كلّ شهرٍ مدة ستة أيامٍ لا تصلّي ولا تصوم، فإذا انقضت اغتسلت وصلت وصامت.
وكيفية الصلاة لهذه وأمثالها: أنّها تغسل فرجها غسلًا تامًّا، وتعصبه، وتتوضأ، وتفعل ذلك بعد دخول وقت صلاة الفريضة، وكذلك تفعله إذا أرادت أن تتنفل في غير أوقات فرائض.
وفي هذه الحال -ومن أجل المشقة عليها- يجوز لها أن تجمع صلاة الظّهر مع العصر، وصلاة المغرب مع العشاء؛ حتى يكون عملها هذا واحدًا للصلاتين: صلاة الظّهر، والعصر.
وواحدًا للصلاتين: صلاة المغرب، والعشاء، وواحدًا لصلاة الفجر، بدلًا من أن تعمل ذلك خمس مراتٍ تعمله ثلاث مراتٍ.
وأعيده مرةً ثانيةً، فأقول: عندما تريد الطهارة تغسل فرجها، وتعصبه بخرقةٍ أو شبهها حتى يخف الخارج، ثم تتوضأ، وتصلّي الظّهر أربعًا، والعصر أربعًا، والمغرب ثلاثًا، والعشاء أربعًا، والفجر ركعتين، أي: أنها لا تقصر، كما يتوهمه بعض العامة،
ولكن يجوز لها أن تجمع بين صلاتي الظّهر والعصر، وبين صلاتي المغرب والعشاء، الظّهر مع العصر إمّا تأخيرًا أو تقديمًا، وكذلك المغرب مع العشاء إما تقديمًا أو تأخيرًا، وإذا أرادت أن تتنفل بهذا الوضوء فلا حرج عليها.