Iwapo imeingia kwangu desturi ya mwezi (hedhi) na hali nikiwa katikati ya swala, nitatakiwa kufanya nini? Na je, nitawajibika kulipa swala hiyo baada ya muda wa hedhi?
السؤال
Swali la 1:
Iwapo imeingia kwangu desturi ya mwezi (hedhi) na hali nikiwa katikati ya swala, nitatakiwa kufanya nini? Na je, nitawajibika kulipa swala hiyo baada ya muda wa hedhi?
س32: دخلت عليّ العادة الشهرية أثناء الصلاة، ماذا أفعل؟ وهل أقضي الصلاة عن مدة الحيض؟
الجواب
Jawabu la 1:
Ikiwa mwanamke itamtokea hedhi baada ya kuingia wakati wa swala; kwa mfano mwanamke akafikwa na hedhi baada ya kupinduka jua kwa nusu saa, basi bila shaka baada ya kutwaharika kutokana na hedhi yake atailipa swala hii ambayo uliingia muda wake na hali akiwa na twahara.
Na hiyo ni kwa mujibu wa kauli ya Allah Mtukufu: "..Kwa hakika swala imekuwa juu ya waumini ni faradhi iliyopangiwa wakati maalumu" [An-Nisai: 103]
Na wala mwanamke hatolipa swala zilizomkuta akiwa ndani ya hedhi; kwa mujibu wa kauli ya Mtume rehema na amani za Allah zimfikie - katika hadithi ndefu:
"Je, si pale mwanamke anapoingia katika hedhi haswali na wala hafungi?"
Na wanachuoni wamekubaliana kuwa mwanamke halipi swala ambayo ilimpita akiwa katika hedhi.
Ama ikiwa atatwaharika, na hali ilikuwa imebaki katika muda wa swala kiasi cha rakaa moja na zaidi, basi ataswali swala hiyo ambayo ni ya wakati aliotwaharika ndani yake, na hii ni kwa mujibu wa kauli yake Mtume rehema na amani za Allah zimfikie:
"Atakayeupata wakati wa swala ya Alasiri kwa kiwango cha rakaa moja kabla jua halijazama basi ameipata Lasiri",
Na ikiwa mwanamke atatwaharika ndani ya wakati wa Alasiri, au kabla ya kuchomoza jua, na ikawa imebaki kabla ya kuzama jua au kuchomoza jua kwa kiasi cha rakaa moja, basi ataswali Alasiri kwa mnasaba wa swala la kwanza, na ataswali Alfajiri kwa mnasaba wa swala la pili.
ﺟ32: إذا حدث الحيض بعد دخول وقت الصلاة -كأن حاضت بعد الزوال بنصف ساعةٍ مثلًا- فإنها بعد أن تطهر من الحيض تقضي هذه الصلاة التي دخل وقتها وهي طاهرٌ؛ لقوله تعالى:
﴿...إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ كَانَتۡ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ كِتَٰبٗا مَّوۡقُوتٗا﴾
[النساء:103].
ولا تقضي الصلاة عن وقت الحيض؛ لقوله ﷺ في الحديث الطويل:
«أَلَيْسَتْ إِذَا حَاضَتْ لَمْ تُصَلِّ، وَلَمْ تَصُمْ؟» [1]،
وأجمع أهل العلم أنها لا تقضي الصلاة التي فاتتها أثناء مدة الحيض.
[12] تقدم تخريجه.
أما إذا طهرت، وكان باقيًا من الوقت مقدار ركعةٍ فأكثر، فإنها تصلّي ذلك الوقت الذي طهرت فيه؛ لقوله ﷺ:
«مَنْ أَدْرَكَ رَكْعَةً مِنَ الْعَصْرِ قَبْلَ أَنْ تَغْرُبَ الشَّمْسُ، فَقَدْ أَدْرَكَ الْعَصْرَ» [2]،
فإذا طهرت وقت العصر، أو قبل طلوع الشمس، وكان باقيًا على غروب الشمس أو طلوعها مقدار ركعةٍ، فإنها تصلّي العصر في المسألة الأولى، والفجر في المسألة الثانية.
[13] تقدم تخريجه.