Nini hukumu ya mwanamke kukaa katika msikiti mtukufu wa Makka au msikiti wa Madina, na hali akiwa na hedhi; kwa nia ya kusikiliza mafunzo ya hadithi za Mtume rehema na amani za Allah zimfikie, na kusikiliza hotuba?
السؤال
Swali la 1:
Nini hukumu ya mwanamke kukaa katika msikiti mtukufu wa Makka au msikiti wa Madina, na hali akiwa na hedhi; kwa nia ya kusikiliza mafunzo ya hadithi za Mtume rehema na amani za Allah zimfikie, na kusikiliza hotuba?
س34: ما حكم وجود المرأة في المسجد الحرام وهي حائضٌ؛ لاستماع الأحاديث والخطب؟
الجواب
Jawabu la 1:
Haijuzu kwa mwanamke mwenye hedhi kukaa ndani ya msikiti wa Makka au msikiti mwingine wowote, lakini inajuzu kwake kupita na kukatisha ndani ya msikiti kwa nia ya kutimiza haja yake humo, na mfano wa hilo;
kama alivyosema Mtume rehema na amani za Allah zimfikie, alipomuamrisha mama Aisha alete Msala, mama Aisha akasema: Msala uko msikitini na mimi nina hedhi. Mtume wa Allah rehema na amani zimfikie akasema: "Hedhi yako haiko mkononi mwako",
Na ikiwa mwanamke mwenye hedhi atakatisha msikitini, na hali ya kuwa damu yake haichuruziki ndani ya msikiti, basi hapana ubaya wowote juu yake.
Neno "Khumra" lililotumika katika hadithi: Ni Mswala unaotumika kuswalia. Na Mswala huo umeitwa hivyo kwa sababu unafunika uso.
Ama ikiwa mwanamke huyo anataka tu kukaa msikitini hilo halitajuzu kisheria.
Na dalili ya hilo: Ni kuwa Mtume rehema na amani za Allah zimfikie aliwaamrisha wanawake kutoka katika swala ya iddi ili kuhudhuria mahala pa tukio la swala ya iddi (wanawake walioachwa huru kutokana na utumwa na mabinti wanaotawa na wanawake wenye hedhi) isipokuwa tu akaamrisha wenye hedhi wajitenge na mahala pa kuswalia.
Hivyo hilo linajulisha kuwa mwanamke mwenye hedhi haijuzu kwake kukaa msikitini kwa nia ya kusikiliza hotuba au kusikiliza darasa na hadithi.
ﺟ34: لا يجوز للمرأة الحائض أن تمكث في المسجد الحرام ولا غيره من المساجد، ولكن يجوز لها أن تمر بالمسجد، وتأخذ الحاجة منه وما أشبه ذلك؛ كما قال النبيّ ﷺ لعائشة حين أمرها أن تأتي بالخمرة[1]، فقالت: إنها في الـمسجد، وإنّي حائضٌ، فقال:
«إِنَّ حَيْضَتَكِ لَيْسَتْ فِي يَدِكِ» [2]،
فإذا مرت الحائض في المسجد، وهي آمنةٌ من أن ينزل دمٌ على المسجد، فلا حرج عليها.
[14] الخمرة: هي السجادة يسجد عليها المصلي، وسميت خمرة؛ لأنها تخمر الوجه، أي: تغطيه.
[15] مسلم، كتاب الحيض، باب جواز غسل الحائض رأس زوجها وترجيله (11) (298).
أما إن كانت تريد أن تدخل وتجلس فهذا لا يجوز.
والدليل على ذلك: أن النبي ﷺ أمر النّساء في صلاة العيد أن يخرجن إلى مصلى العيد -العواتق، وذوات الخدور، والحيض- إلا أنه أمر أن يعتزل الحيض المصلى [3]،
فدل ذلك على أنّ الحائض لا يجوز لها أن تمكث في المسجد لاستماع الخطبة، أو استماع الدرس والأحاديث.
[16] البخاري، كتاب العيدين، باب خروج النساء والحيض (974)، ومسلم، كتاب العيدين، باب ذكر إباحة خروج النساء في العيدين إلى المصلى (10) (890).
من أحكام الطهارة في الصلاة