Je kinachotoka kwa kuchuruzika toka kwa mwanamke (katika sehemu zake za siri)- kikiwa ni rangi nyeupe au ya njano- ni najisi au twahara, na je unawajibika udhu kwa hicho kinachotoka, pamoja na kujuwa kwamba kinaendelea kutoka bila kukatika, na ipi hukumu ikiwa kitaacha kutoka? hususani ni kwamba wengi katika wanawake wasomi wanazingatia kile kinachotoka ni unyevunyevu wa kawaida na wa asili, hailazimiki kuchukua Udhu?
السؤال
Swali la 1:
Je kinachotoka kwa kuchuruzika toka kwa mwanamke (katika sehemu zake za siri)- kikiwa ni rangi nyeupe au ya njano- ni najisi au twahara, na je unawajibika udhu kwa hicho kinachotoka, pamoja na kujuwa kwamba kinaendelea kutoka bila kukatika, na ipi hukumu ikiwa kitaacha kutoka? hususani ni kwamba wengi katika wanawake wasomi wanazingatia kile kinachotoka ni unyevunyevu wa kawaida na wa asili, hailazimiki kuchukua Udhu?
س35: هل السائل الّذي ينزل من المرأة -أبيض كان أم أصفر- طاهرٌ أو نجسٌ؟ وهل يجب فيه الوضوء، مع العلم بأنه ينزل مستمرًّا؟ وما الحكم إذا كان متقطّعًا، خاصةً أن غالب النّساء -لا سيما المتعلّمات- يعتبرن ذلك رطوبةً طبيعيةً، لا يلزم منه الوضوء؟
الجواب
Jawabu la 1:
Kinachodhihiri kwangu baada ya utafiti ni kuwa: Kinachochuruzika kutoka kwa mwanamke ikiwa hakitoki kwenye kibofu basi kinatoka katika mfuko wa uzazi na kitakuwa ni twahara, lakini kinatengua udhu pamoja na kuwa ni twahara: Kwa sababu kitu kinachotengua udhu si sharti kiwe najisi, kwani huoni upepo unaotoka sehemu ya nyuma hauna umbo, lakini pamoja na hivyo unatengua udhu.
Na kwa ajili hiyo tu, ikiwa damu hiyo itamtoka mwanamke na hali akiwa na udhu basi damu hiyo itatengua udhu wake, na itamuwajibikia kutawadha udhu mpya.
Na ikiwa damu hiyo inaendelea kutoka haitatengua udhu wake, lakini atatawadha kwa ajili ya swala pindi utakapoingia muda wake, na kwa udhu huo huo ataswali swala ya sunna na atasoma Qur'ani, na atafanya lolote katika mambo ya halali kwake.
Na hivi ni kama walivyosema wasomi kuhusu mtu mwenye ugonjwa wa kutokwa na mkojo mfululizo, hii ndiyo hukumu ya mwenye kutokwa na damu katika kadhia ya twahara, anakuwa twahara, na katika swala la kutenguka udhu wake, mkojo huo unatengua udhu ila tu ikiwa unatoka mfululizo wakati huo hautatengua udhu. Lakini mwanamke hatatawadha kwa ajili ya swala ila baada ya kuingia muda, na awe muangalifu.
Ama ikiwa damu hiyo inakatika, na ikawa desturi yake haikatiki katika nyakati za swala, basi ataahirisha swala mpaka wakati ambao damu inakatika, madhali tu hahofii kupitwa na kipindi cha swala. Ikiwa atahofia kupitwa na kipindi cha swala basi itambidi atawadhe na atajifunga na kujihifadhi na kuswali.
Na hapana tofauti kati ya damu ndogo na damu nyingi; Kwa sababu zote hizo zinatokea katika njia moja; hivyo basi ikiwa ni nyingi au kidogo zote hizo zinatengua udhu. Hii ni tofauti na damu inayotoka katika maeneo mengine ya mwili kama damu au matapishi, vitu hivyo havitengui udhu vikiwa kidogo au vikiwa vingi.
Ama itikadi ya baadhi ya wanawake kuhusu damu hiyo kwamba haitengui udhu hili mimi sijui linatokana na asili ipi, isipokuwa kauli ya Ibn Hazmi Allah amrehemu yeye anasema: Damu hii haitengui udhu, lakini hakuleta dalili yoyote juu ya kauli yake hii na lau angetaja dalili yoyote kutoka katika kitabu na sunna na kauli za Maswahaba hiyo ingelikuwa ni hoja.
Na ni juu ya mwanamke kumcha Allah na apupie kujitwaharisha; kwa sababu swala haikubaliwi bila ya twahara, hata akiswali mara mia, kwani baadhi ya wanachuoni wanasema: Mtu anayeswali bila ya twahara anafanya kufuru; kwa sababu kufanya hivyo ni kuzifanyia kejeli aya za Allah -Aliyetakasika na Kutukuka.
ﺟ35: الظاهر لي بعد البحث: أن السائل الخارج من المرأة إذا كان لا يخرج من المثانة، وإنما يخرج من الرحم، أنّه طاهرٌ، ولكنه ينقض الوضوء وإن كان طاهرًا؛ لأنه لا يشترط للناقض للوضوء أن يكون نجسًا، فها هي الرّيح تخرج من الدّبر، وليس لها جرمٌ، ومع ذلك تنقض الوضوء.
وعلى هذا، إذا خرج من المرأة وهي على وضوءٍ فإنه ينقض الوضوء، وعليها تجديده.
فإن كان مستمرًّا فإنه لا ينقض الوضوء، ولكن تتوضأ للصلاة إذا دخل وقتها، وتصلّي في هذا الوقت الّذي تتوضأ فيه فروضًا ونوافل، وتقرأ القرآن، وتفعل ما شاءت ممّا يباح لها،
كما قال أهل العلم نحو هذا فيمن به سلس البول، هذا هو حكم السائل من جهة الطهارة، فهو طاهرٌ، ومن جهة نقضه للوضوء، فهو ناقضٌ للوضوء إلا أن يكون مستمرًّا عليها، فإن كان مستمرًّا فإنه لا ينقض الوضوء، لكن على المرأة ألا تتوضأ للصلاة إلا بعد دخول الوقت، وأن تتحفظ.
أما إن كان منقطعًا، وكان من عادته أن ينقطع في أوقات الصلاة، فإنها تؤخّر الصلاة إلى الوقت الّذي ينقطع فيه، ما لم تخش خروج الوقت، فإن خشيت خروج الوقت فإنها تتوضأ، وتتلجم -تتحفظ- وتصلّي.
ولا فرق بين القليل والكثير؛ لأنه كله خارجٌ من السبيل، فيكون ناقضًا قليله وكثيره، بخلاف الذي يخرج من بقية البدن كالدم والقيء، فإنه لا ينقض الوضوء، لا قليله ولا كثيره.
وأما اعتقاد بعض النّساء أنه لا ينقض الوضوء فهذا لا أعلم له أصلًا، إلا قولًا لابن حزمٍ رحمه الله، فإنه يقول: إن هذا لا ينقض الوضوء، ولكنه لم يذكر لهذا دليلًا، ولو كان له دليلٌ من الكتاب والسّنة أو أقوال الصحابة لكان حجةً.
وعلى المرأة أن تتقي الله، وتحرص على طهارتها؛ فإن الصلاة لا تقبل بغير طهارةٍ ولو صلت مئة مرةٍ، بل إن بعض العلماء يقول: إن الذي يصلّي بلا طهارةٍ يكفر؛ لأن هذا من باب الاستهزاء بآيات الله سبحانه وتعالى.