Skip to content
Orodha ya Sura /

يسٓ

يسٓ is chapter 36 of the Quran and has 83 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

83 Aya Sura Na. 36
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

يسٓ

Ya-Sin (Y.S.).

Explanation & meanings · 1
  1. Ya-Sin: Hizi ni harufi mbili zilizo anzia Sura hii kwa mujibu wa mpango wa Qur'ani katika kuanzia baadhi ya Sura kwa harufi moja moja.

وَٱلۡقُرۡءَانِ ٱلۡحَكِيمِ

Kwa Haki ya Qur'ani yenye hikima!

Explanation & meanings · 1
  1. Ninaapa kwa Qur'ani yenye kukusanya hikima na ilimu yenye manufaa.

إِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Hakika wewe ni miongoni mwa walio tumwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika wewe, Muhammad, ni katika wale ambao Mwenyezi Mungu amewatuma kwa watu wawapelekee Uwongofu na Dini ya Haki.

عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Juu ya Njia Iliyo Nyooka.

Explanation & meanings · 1
  1. Juu ya Njia Iliyo Sawa, nayo ndiyo Dini ya Kiislamu.

تَنزِيلَ ٱلۡعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ

Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.

Explanation & meanings · 1
  1. Ni mteremsho wa Mwenye nguvu Mwenye kushinda kila kitu, ambaye hapana mtu awezae kumzuia chochote akitakacho. Mwenye kuwarehemu waja wake, kwa kuwatumia watu wa kuwaongoza njia ya kuokoka.