36 : 45
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّقُواْ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيكُمۡ وَمَا خَلۡفَكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
Na wanapo ambiwa: Jilindeni na yalioko mbele yenu na yalioko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa
Explanation & meanings · 1
- Na wanapo ambiwa: Yaogopeni mfano wa yaliyo wapata mataifa yaliyo kwisha pita kwa kukadhibisha kwao, na iogopeni adhabu ya Akhera ambayo itakupateni kwa kushikilia kwenu ukafiri, kwa kutaraji kuwa asaa Mola wenu Mlezi akakurehemuni mkimcha Yeye, wao hupuuza.