36 : 26
قِيلَ ٱدۡخُلِ ٱلۡجَنَّةَۖ قَالَ يَٰلَيۡتَ قَوۡمِي يَعۡلَمُونَ
Akaambiwa: Ingia Peponi! Akasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua
Explanation & meanings · 1
- Kuwa ni malipo ya Imani yake na wito wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ataambiwa: Ingia Peponi! Naye, hali yuko katika kivuli cha neema na hishima, atasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua alivyo nighufiria Mola wangu Mlezi na kunipa hishima, nao wakaamini kama nilivyo amini mimi.