Skip to content
يسٓ /

Aya 78

36 : 78

Aya 78 of يسٓ (36 : 78). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يسٓ Aya 83
Sura · يسٓ
Kiswahili · Barawani
36 : 78

وَضَرَبَ لَنَا مَثَلٗا وَنَسِيَ خَلۡقَهُۥۖ قَالَ مَن يُحۡيِ ٱلۡعِظَٰمَ وَهِيَ رَمِيمٞ

Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika?

Explanation & meanings · 1
  1. Tena huyu mpingaji aliye dhaahiri ametupigia mfano ambao kwao anakanya uweza wetu kufufua mafupa baada ya kuoza na kusagika. Na amesahau kuwa Sisi tulimuumba yeye, naye hata hakuwepo aslani. Akasema kwa kukanya na kuona haliwezi kuwa hilo: Ni nani huyo atakaye yafufua mafupa nayo yamekwisha mung'unyika?