Skip to content

Mimi nilikwenda Umra, nilipita katika eneo la kuhirimia na kutia nia ya ibada hiyo nikiwa katika hedhi, sikuhirimia, nikabakia katika mji wa Makka mpaka nikatwaharika, nikahirimia katika mji wa Makka, je jambo hili linafaa? na nini natakiwa kufanya, na ni lipi ninawajibika kwalo?

السؤال

Swali la 1:

Mimi nilikwenda Umra, nilipita katika eneo la kuhirimia na kutia nia ya ibada hiyo nikiwa katika hedhi, sikuhirimia, nikabakia katika mji wa Makka mpaka nikatwaharika, nikahirimia katika mji wa Makka, je jambo hili linafaa? na nini natakiwa kufanya, na ni lipi ninawajibika kwalo?

س54: أنا ذاهبةٌ للعمرة، ومررت بالميقات وأنا حائضٌ، فلم أحرم، وبقيت في مكة حتّى طهرت، فأحرمت من مكة، فهل هذا جائزٌ؟ أو ماذا أفعل؟ وما يجب عليّ؟

الجواب

Jawabu la 1:

Kitendo kilichofanyika hakiko sahihi, mwanamke anayetaka kufanya Umra, haifai kwake kupita eneo la kuhirimia mpaka atie nia ya kufanya ibada ya Umra/Hija hata akiwa na hedhi, kutia nia kwake kuna hesabika na ni sahihi.

Na dalili ya hilo ni kwamba: Alijifungua Asmaa bint Umaisi, mke wa Abubakari -radhi Allah ziwe juu yao- na Mtume- rehema na amani ziwe juu yake- akiwa anashuka katika mji wa Dhul-Hulaifa, alikuwa akikusudia kufanya Hija ya kuaga, akaagiza ujumbe Asmaa kwenda kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- nini anatakiwa afanye katika hali kama hiyo? Akasema:" Koga, kisha zuia na nguo, na hirimia (Tia nia ya ibada ya Hija).

Na damu ya hedhi ni kama damu ya nifasi.

Basi tunasema kwa mwanamke mwenye hedhi atakapopita eneo la kuhirimia (kutia nia), akiwa anataka kufanya Hija au Umra, tunamwambia: Koga, zuia na nguo sehemu ya damu, na hirimia.

Na kujistiri maana yake ni: Aweke vizuri kipande cha nguo katika sehemu yake ya siri ya mbele, na aifunge vizuri nguo hiyo, kisha ahirimie sawa sawa iwe ni ibada ya Hija au Umra, lakini akihirimia na akafika Makka haruhusiwi kuizunguka Kaaba mpaka atwaharike.

Na kwa hili alisema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Aisha pindi alipopata hedhi akiwa katika Umra: "Fanya yote anayoyafanya mwenye kufanya Hija isipokuwa usizunguke Kaaba mpaka Utwaharike", na hii ni riwaya ya Bukhari na Muslim.

Na pia katika -Sahihi Bukhari- ametaja Aisha kwamba alipotwaharika alizunguka Kaaba, na akazunguka mlima wa Swafa na Marwa,

hii ikaonyesha kwamba mwanamke akihirimia kufanya ibada ya Hija au Umra, naye akiwa katika hedhi, au ilimjia hedhi kabla hajazunguka Kaaba, basi hatozunguka Kaaba na kuzunguka Swafa na Marwa mpaka atwaharike na akoge.

Ama akitufu hali ya kuwa ametwaharika, baada ya kumaliza kuzunguka Kaaba ndio ikamjia hedhi, basi ataendelea, na atazunguka Swafa na Marwa hata kama akiwa na hedhi, na atapunguza nywele zake, na Umra yake itamalizika, kwa sababu kuzunguka Swafa na Marwa hakushurutishwi kutwaharika.

ﺟ54: هذا العمل ليس بجائزٍ، والمرأة الّتي تريد العمرة لا يجوز لها مجاوزة الميقات إلا بإحرامٍ حتى لو كانت حائضًا، فإنها تحرم وهي حائضٌ، وينعقد إحرامها، ويصحّ،

والدليل لذلك: أن أسماء بنت عميسٍ زوجة أبي بكرٍ رضي الله عنهما ولدت، والنبيّ ﷺ نازلٌ في ذي الحليفة، يريد حجة الوداع، فأرسلت إلى النبيّ ﷺ: كيف أصنع؟ قال:

«اغْتَسِلِي، وَاسْتَثْفِرِي بِثَوْبٍ، وَأَحْرِمِي» [1]،

ودم الحيض كدم النّفاس.

[24] تقدم تخريجه.

فنقول للمرأة الحائض إذا مرت بالميقات، وهي تريد العمرة أو الحج نقول لها: اغتسلي، واستثفري بثوبٍ، وأحرمي،

والاستثفار معناه: أنها تشدّ على فرجها خرقةً، وتربطها، ثم تحرم، سواء بالحجّ أو بالعمرة، ولكنها إذا أحرمت ووصلت إلى مكة لا تأتي إلى البيت، ولا تطوف به حتى تطهر، ولهذا قال النبيّ ﷺ لعائشة حين حاضت في أثناء العمرة، قال لها:

«افْعَلِي مَا يَفْعَلُ الْحَاجُّ، غَيْرَ أَلَّا تَطُوفِي فِي الْبَيْتِ حَتَّى تَطْهُرِي» [2]،

هذه رواية البخاريّ ومسلمٍ، وفي «صحيح البخاريّ» أيضًا،

«ذَكَرَتْ عَائِشَةُ أَنَّهَا لَمَّا طَهُرَتْ طَافَتْ بِالْبَيْتِ، وَبِالصَّفَا وَالْمَرْوَةِ» [3]،

فدل هذا على أن المرأة إذا أحرمت بالحجّ أو العمرة وهي حائضٌ، أو أتاها الحيض قبل الطواف، فإنها لا تطوف ولا تسعى حتى تطهر وتغتسل.

[26] البخاري، كتاب العمرة، باب عمرة التنعيم (1785).

[25] رواه البخاري، كتاب الحج، باب تقضي الحائض المناسك كلها إلا الطواف بالبيت (1650)، ومسلم، كتاب الحج، باب بيان وجوه الإحرام (120) (1211).

أما لو طافت وهي طاهرٌ، وبعد أن انتهت من الطواف جاءها الحيض، فإنها تستمرّ، وتسعى ولو كان عليها الحيض، وتقصّ من رأسها، وتنهي عمرتها؛ لأنّ السعي بين الصفا والمروة لا يشترط له الطهارة.