Skip to content

Nimefika toka Yanbu'i kwa ajili ya Umra mimi na familia yangu, lakini nilivyofika Jidda, akapambazukiwa na asubuhi mke wangu akiwa na hedhi, nikakamilisha Umra peke yangu bila ya mke wangu kufanya Umra yake, ni ipi hukumu kuhusu mke wangu?

السؤال

Swali la 1:

Nimefika toka Yanbu'i kwa ajili ya Umra mimi na familia yangu, lakini nilivyofika Jidda, akapambazukiwa na asubuhi mke wangu akiwa na hedhi, nikakamilisha Umra peke yangu bila ya mke wangu kufanya Umra yake, ni ipi hukumu kuhusu mke wangu?

س55: لقد قدمت من ينبع للعمرة أنا وأهلي، ولكن حين وصولي إلى جدة أصبحت زوجتي حائضًا، ولكنّي أكملت العمرة بمفردي دون زوجتي، فما الحكم بالنّسبة لزوجتي؟

الجواب

Jawabu la 1:

Hukumu kwa kumzingatia mke wako, ni kusubiri mpaka atwaharike, kisha akamilishe Umra yake;

Kwa sababu Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-pindi Swafia- radhi za Allah ziwe juu yake- alipopata hedhi akasema: "Je itatuzuia sisi hiyo?", Wakasema: Hakika yeye alikwisha zunguka kaaba kwa ajili ya Hija, akasema: "Basi na aendelee".

Kauli yake -rehema na amani ziwe juu yake-: "Je itatuzuia sisi hiyo?", Hii ni dalili ya kuwa mwanamke anatakiwa abakie akipata damu ya hedhi kabla ya kuzunguka Kaaba kwa ajili ya Hija, mpaka atwaharike kisha azunguke.

Hivyo hivyo kuzunguka Kaaba kwa ajili ya Umra ni mfano wa kuzunguka Kaaba kwa ajili ya Hija (Al-ifadhah), kwa sababu mzunguko huo ni nguzo, anapopata hedhi anayefanya ibada ya Umra kabla ya kuzunguka Kaaba basi atasubiri mpaka atwaharike kisha azunguke Kaaba.

ﺟ55: الحكم بالنّسبة لزوجتك: أن تبقى حتى تطهر، ثم تقضي عمرتها؛ لأن النبي ﷺ لـما حاضت صفية رضي الله عنها قال:

«أَحَابِسَتُنَا هِيَ؟» قَالُوا: إِنَّهَا قَدْ أَفَاضَتْ. قَالَ: «فَلْتَنْفِرْ إِذًا» [1]،

فقوله ﷺ: «أحابستنا هي؟» دليلٌ على أنه يجب على المرأة أن تبقى -إذا حاضت قبل طواف الإفاضة- حتى تطهر، ثمّ تطوف.

[27] تقدم تخريجه.

وكذلك طواف العمرة مثل طواف الإفاضة؛ لأنه ركنٌ من العمرة، فإذا حاضت المعتمرة قبل الطواف انتظرت حتى تطهر، ثم تطوف.