Je eneo la kuzunguka Swafa na Marwa ni eneo takatifu? Je mwenye hedhi atasogelea eneo hilo? Je anawajibika yule atakayeingia katika eneo takatifu la kuzunguka Swafa na Marwa aswali rakaa mbili za kusalimia msikiti?
السؤال
Swali la 1:
Je eneo la kuzunguka Swafa na Marwa ni eneo takatifu? Je mwenye hedhi atasogelea eneo hilo? Je anawajibika yule atakayeingia katika eneo takatifu la kuzunguka Swafa na Marwa aswali rakaa mbili za kusalimia msikiti?
س56: هل المسعى من الحرم؟ وهل تقربه الحائض؟ وهل يجب على من دخل الحرم من المسعى أن يصلّي تحية المسجد؟
الجواب
Jawabu la 1:
Ambalo linadhihiri eneo la kuzunguka Swafa na Marwa sio katika msikiti mtukufu, na ndio maana wameweka ukuta wenye kutenganisha baina ya msikiti na eneo la kuzunguka Swafa na Marwa, lakini ni ukuta mfupi, na hakuna shaka kwamba jambo hili ni bora kwa watu, kwa sababu lau eneo hilo lingeingizwa na kuwa katika Msikiti, angekuwa mwanamke akipata damu ya hedhi na kamaliza kutufu bado kuzunguka Swafa na Marwa angezuiliwa kuzunguka kwa sababu eneo la kuzunguka ni katika Msikiti, na mwanamke mwenye hedhi haruhusiwi kuwa humo.
Jambo ambalo ninalitolea Fatwa katika hili ni: Akipata hedhi baada kuzunguka Kaaba na kabla ya kuzunguka Swafa na Marwa, basi anaruhusiwa kuzunguka, kwa sababu sehemu ya kuzunguka Swafa na Marwa haizingatiwi kama ipo ndani ya msikiti.
Ama rakaa mbili za kuusalimia msikiti kunaweza kusemwa kuwa: Mtu akizunguka Swafa na Marwa baada ya kuzunguka Kaaba, kisha akarudi msikitini, basi ataziswali, na akiacha kuswali hana dhambi.
Na lililo bora ni kuitumia fursa vizuri, na aswali rakaa mbili, kwa sababu kuswali maeneo kama hayo kuna fadhila kubwa.
ﺟ56: الّذي يظهر أن المسعى ليس من المسجد، ولذلك جعلوا جدارًا فاصلًا بينهما، لكنه جدارٌ قصيرٌ، ولا شك أن هذا خيرٌ للناس؛ لأنه لو أدخل في المسجد وجعل منه، لكانت المرأة إذا حاضت بين الطواف والسعي امتنع عليها أن تسعى.
والّذي أفتي به: أنها إذا حاضت بعد الطواف وقبل السعي فإنها تسعى؛ لأن المسعى لا يعتبر من المسجد.
وأما تحية المسجد فقد يقال: إن الإنسان إذا سعى بعد الطواف، ثم عاد إلى المسجد، فإنه يصلّيها، ولو ترك تحية المسجد فلا شيء عليه،
والأفضل أن ينتهز الفرصة، ويصلّي ركعتين؛ لـما في الصلاة في هذا المكان من الفضل.