بَرَآءَةٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦٓ إِلَى ٱلَّذِينَ عَٰهَدتُّم مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Huku ni kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwenye jukumu la maagano na mlio ahidiana nao katika washirikina.
- Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajitoa katika dhima, wala jukumu lolote, na wale washirikina mlio peana nao ahadi, na wao wakavunja hayo mlio ahidiana nao.