9 : 76
فَلَمَّآ ءَاتَىٰهُم مِّن فَضۡلِهِۦ بَخِلُواْ بِهِۦ وَتَوَلَّواْ وَّهُم مُّعۡرِضُونَ
Alipo wapa katika fadhila yake wakaifanyia ubakhili na wakageuka, na huku wakipuuza.
Explanation & meanings · 1
- Mwenyezi Mungu akiwaitikia na akawapa kwa fadhila yake, wanafanya ubakhili. Hawatoi kitu, wala hawatimizi ahadi, na huiacha kheri wakiipuuza na wakimpuuza Mwenyezi Mungu.