Skip to content
At-Tawbah /

Aya 95

9 : 95

Aya 95 of At-Tawbah (9 : 95). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

At-Tawbah Aya 129
Sura · At-Tawbah
Kiswahili · Barawani
9 : 95

سَيَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمۡ إِذَا ٱنقَلَبۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡ لِتُعۡرِضُواْ عَنۡهُمۡۖ فَأَعۡرِضُواْ عَنۡهُمۡۖ إِنَّهُمۡ رِجۡسٞۖ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُ جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Watakuapieni kwa Mwenyezi Mungu mtakapo rudi kwao ili muwaachilie mbali. Basi waachilieni mbali. Hakika hao ni najsi, na makaazi yao ni Jahannamu, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyachuma.

Explanation & meanings · 1
  1. Watakuapieni kwa Mwenyezi Mungu pale mtapo rejea kwao, kwamba wao wanasema kweli katika kutoa udhuru wao, ili muwaridhie na kwa hivyo waghafilike na vitendo vyao. Basi msiwakubalie kwa lengo lao hilo. Bali watengeni na muwachukie, kwani wao wako daraja ya mwisho kabisa ya ukhabithi wa roho na ukafiri. Na mwisho wao ni Jahannamu, kuwa ndio adabu yao kwa madhambi na maasi walio yatenda!