Skip to content
التوبَة /

Aya 93

9 : 93

Aya 93 of التوبَة (9 : 93). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

التوبَة Aya 129
Sura · التوبَة
Kiswahili · Barawani
9 : 93

۞ إِنَّمَا ٱلسَّبِيلُ عَلَى ٱلَّذِينَ يَسۡتَـٔۡذِنُونَكَ وَهُمۡ أَغۡنِيَآءُۚ رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ ٱلۡخَوَالِفِ وَطَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Ipo njia ya kuwalaumu wale wanao kuomba ruhusa wasende vitani na hali wao ni matajiri. Wameridhia kuwa pamoja na wanao bakia nyuma. Na Mwenyezi Mungu amewapiga muhuri juu ya nyoyo zao. Kwa hivyo hawajui.

Explanation & meanings · 1
  1. Lawama na adhabu ni juu ya wale wanao kutaka ruhusa, ewe Mtume, wabakie nyuma wasende vitani, nao wanayo mali na zana, na wanaweza kutoka pamoja nawe. Kwani hao juu ya uwezo wao wamekhiari wabaki nyuma pamoja na wanawake wanyonge, na wazee wakongwe, na wagonjwa wasio jiweza; na nyoyo zao hao zimefungwa hazitambui Haki, na hawajui matokeo maovu kabisa yatakayotokea duniani na Akhera kwa kule kuacha kutoka kwao kwenda kwenye Jihadi.