Skip to content
التوبَة /

Aya 103

9 : 103

Aya 103 of التوبَة (9 : 103). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

التوبَة Aya 129
Sura · التوبَة
Kiswahili · Barawani
9 : 103

خُذۡ مِنۡ أَمۡوَٰلِهِمۡ صَدَقَةٗ تُطَهِّرُهُمۡ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيۡهِمۡۖ إِنَّ صَلَوٰتَكَ سَكَنٞ لَّهُمۡۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Mtume! Pokea kwa hawa wenye kutubu sadaka zao, uwasafishe kwa hizo sadaka makosa yao na uchoyo wao, na unyanyue daraja zao mbele ya Mwenyezi Mungu. Na waombee kheri na uwongofu; kwani kuomba kwako kutawapoza nafsi zao, na zitatulia nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia maombi, Mwenye kuwajua wenye nyoyo safi katika toba zao.