9 : 27
ثُمَّ يَتُوبُ ٱللَّهُ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ عَلَىٰ مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Kisha baada ya hayo Mwenyezi Mungu atawasamehe awatakao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
Explanation & meanings · 1
- Kisha Mwenyezi Mungu atakubali toba ya amtakaye katika waja wake, na amsamehe dhambi zake, pindi akirejea kwa usafi wa moyo. Na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa kusamehe, Mkuvunjufu wa kurehemu.