Skip to content
التوبَة /

Aya 122

9 : 122

Aya 122 of التوبَة (9 : 122). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

التوبَة Aya 129
Sura · التوبَة
Kiswahili · Barawani
9 : 122

۞ وَمَا كَانَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ لِيَنفِرُواْ كَآفَّةٗۚ فَلَوۡلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرۡقَةٖ مِّنۡهُمۡ طَآئِفَةٞ لِّيَتَفَقَّهُواْ فِي ٱلدِّينِ وَلِيُنذِرُواْ قَوۡمَهُمۡ إِذَا رَجَعُوٓاْ إِلَيۡهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَحۡذَرُونَ

Wala haiwafalii Waumini kutoka wote. Lakini kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakapo warejea, ili wapate kujihadharisha?.

Explanation & meanings · 1
  1. Haifai Waumini watoke wote kwenda kwa Mtume s.a.w. ila iwe dharura. Itakikanavyo ni kutoka kikundi kwenda kwa Mtume kwa ajili ya kusoma Dini, na wapate kuwaita watu wao kuwaonya na kuwabashiria, pale wanapo rejea. Haya ili wapate kuwa imara daima juu ya Haki, na watahadhari na upotovu na uharibifu.