Skip to content
التوبَة /

Aya 114

9 : 114

Aya 114 of التوبَة (9 : 114). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

التوبَة Aya 129
Sura · التوبَة
Kiswahili · Barawani
9 : 114

وَمَا كَانَ ٱسۡتِغۡفَارُ إِبۡرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوۡعِدَةٖ وَعَدَهَآ إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُۥٓ أَنَّهُۥ عَدُوّٞ لِّلَّهِ تَبَرَّأَ مِنۡهُۚ إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ لَأَوَّٰهٌ حَلِيمٞ

Wala haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake ila kwa sababu wa ahadi aliyo fanya naye. Lakini ilipo mbainikia kwamba yeye ni adui ya Mwenyezi Mungu, alijiepusha naye. Hakika Ibrahim alikuwa mwingi wa kuomba, mnyenyekevu, mvumilivu.

Explanation & meanings · 1
  1. Haikuwa vile alivyo fanya Ibrahim a.s. kumtakia msamaha baba yake ila ni kutimiza ahadi aliyo ahidi Ibrahim kumuahidi baba yake, kwa kutaraji kuwa atakuja amini. Ilipo kwisha mbainikia Ibrahim kuwa huyo ni adui wa Mwenyezi Mungu kwa kushikilia kwake ushirikina mpaka akafa na ukafiri, Ibrahim alijitenga naye, na akaacha kumwombea maghfira. Na Ibrahim alikuwa mwingi wa kuomba, na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, na mstahamilivu kwa maudhi.