Skip to content
التوبَة /

Aya 35

9 : 35

Aya 35 of التوبَة (9 : 35). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

التوبَة Aya 129
Sura · التوبَة
Kiswahili · Barawani
9 : 35

يَوۡمَ يُحۡمَىٰ عَلَيۡهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكۡوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمۡ وَجُنُوبُهُمۡ وَظُهُورُهُمۡۖ هَٰذَا مَا كَنَزۡتُمۡ لِأَنفُسِكُمۡ فَذُوقُواْ مَا كُنتُمۡ تَكۡنِزُونَ

Siku zitapo tiwa moto katika Moto wa Jahannamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mlio jilimbikia nafsi zenu, basi onjeni mliyo kuwa mkilimbika.

Explanation & meanings · 1
  1. -- Siku ya Kiyama, kwa kuwa hayo mali yatatiwa kwenye Moto wa Jahannamu, kisha waunguzwe nayo kwenye vipaji vya nyuso zao, na mbavu zao, na migongo yao; na waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkijilimbikia kama khazina kwa ajili ya nafsi zenu, wala hamkuwa mkitoa haki ya Mwenyezi Mungu! Basi ionjeni hii leo adhubu kali!