9 : 82
فَلۡيَضۡحَكُواْ قَلِيلٗا وَلۡيَبۡكُواْ كَثِيرٗا جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Basi nawacheke kidogo; watalia sana. Hayo ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.
Explanation & meanings · 1
- Basi nawacheke kufurahia kutokwenda vitani na kuwakejeli Waumini. Kwani kicheko chao muda wake ni mfupi; kitakwisha yatakapo kwisha maisha yao hapa duniani. Tena kitafuata kilio kikubwa kisicho kuwa na mwisho cha huko Akhera. Hayo ni malipo yao kwa madhambi waliyo yafanya.