Skip to content
Orodha ya Sura /

المَعَارج

المَعَارج is chapter 70 of the Quran and has 44 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

44 Aya Sura Na. 70
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

سَأَلَ سَآئِلُۢ بِعَذَابٖ وَاقِعٖ

Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea!

Explanation & meanings · 1
  1. Ameita, mwenye kuita, kuhimiza kama kufanya kejeli, iletwe upesi adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo hapana shaka itawashukia makafiri.

لِّلۡكَٰفِرِينَ لَيۡسَ لَهُۥ دَافِعٞ

Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia .

Explanation & meanings · 1
  1. Wala hapana chochote cha kuzuia adhabu hiyo,

مِّنَ ٱللَّهِ ذِي ٱلۡمَعَارِجِ

Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja.

Explanation & meanings · 1
  1. Kwani hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu, ambako huko ndiko zinatoka nguvu zinazo simama, na hukumu inayo tekelezwa.

تَعۡرُجُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيۡهِ فِي يَوۡمٖ كَانَ مِقۡدَارُهُۥ خَمۡسِينَ أَلۡفَ سَنَةٖ

Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu!

Explanation & meanings · 1
  1. Malaika na Jibrili wanapanda kwenda kunako toka amri yake kwa siku ambayo urefu wake ni miaka khamsini elfu kwa mujibu wa hisabu ya miaka ya duniani.

فَٱصۡبِرۡ صَبۡرٗا جَمِيلًا

Basi subiri kwa subira njema.Hakika wao wanaiona iko mbali!

Explanation & meanings · 1
  1. Basi, ewe Muhammad! Subiri uwastahamilie hizo kejeli zao, na kuhimiza kwao adhabu, kwa subira isiyo kuwa na mbabaiko ndani yake wala mashtaka.